Bahari ya Hindi (Picha ya liblary )
Jioni ya January 31 2013 iliripoti kuhusu kuzama kwa Jahazi liitwalo Sunrise likitokea Tanga kulekea visiwani Zanzibar likiwa na abiria 32 ambapo lilizama kwenye lile eneo la Nungwi .
Polisi Zanzibar walisema “tayari tumeshapokea watu 22 waliookolewa wakiwa wazima na hakuna maiti iliyopatikana mpaka sasa hivi, waliokuwemo kwenye chombo ni watu 32 hivyo watu bado watu 10 hawajulikani walipo”
Baada ya hapo millardayo iliahidiwa tena kuongea na Polisi baadae ili kujua zoezi la uokoaji limefikia wapi, kweli Polisi walitoa tamko lao usiku.
“Oparesheni ilimalizika na hakuna yeyote aliepatikana zaidi ya walewale 22 wa mwanzo ambao walipelekwa hospitali na wote wamesharuhusiwa isipokua nahodha ambae bado amelazwa hospitali kwa matibabu, kimsingi shauri linaendelea na upelelezi na baada ya kukamilika sheria itachukua mkondo wake”
Kwa taarifa hiyo inamaana watu 10 ambao hawakuokolewa mwanzoni wanahofiwa kufa maji manake mpaka oparesheni ya uokoaji imemalizika hawakuonekana, kwa
No comments:
Post a Comment