ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 12, 2012

MJUE MGOMBEA KITI CHA UKATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA-DMV

NDUGU AMOS MATALI CHEREHANI
NI MTANZANIA WA KUZALIWA ANAYEISHI WASHINGTON DC. NI MTAALAM WA MAMBO YA FEDHA NA UTAWALA AMBAYE AMEFANYA KAZI MBALIMBALI HAPA DMV. NI MCHAPAKAZI, MTU ALIYE NA MSIMAMO USIOTINGISHIKA, MWENYE UZOEFU,  BABA WA FAMILIA NA AMBAYE ANAYO MAONO YA KUWEZA KUWAUNGANISHA WATANZANIA WAISHIO HAPA MAREKANI NA WALIOKO TANZANIA.
TUMIA NAFASI YAKO KUCHAGUA KIONGOZI ALIYE NA UPEO WA MASUALA MBALIMBALI YA MAENDELEO ILI APATE NAFASI YA KUSHIRIKIANA NA WATANZANIA WOTE HAPA DMV KULETA MABADILIKO YA KWELI.
CHAGUA MABADILIKO- MCHAGUE NDUGU AMOS MATALI CHEREHANI

20 comments:

Anonymous said...

Sasa watu makini wameanza jitokeza kugombea.Kaka Amos kwa elimu yako,professional yako,uongozi tunauona kanisani kwako,unavyoendesha bishara zako, pata kura yangu bila kinyongo wala kuburuzwa.

Anonymous said...

Ukitaka kujua utamu wa ngoma, ingia mwenyewe ucheze. Hakuna teeena cha mgombea pekee katika nafasi za uongozi. Jiwe la shoka lililobobea kielimu na kimaadili limeingiza timu. Mzee Cherehani nachukua nafasi hii kuku-endorse moja kwa moja nikijua utabadilisha mwelekeo wa upepo ili utufikishe pale ambapo Watanzania tunataka tuwe lakini hatujapata wa kutupeleka. Chukua ticket hii na ingia kwenye mpambano moja kwa moja.

Anonymous said...

Nakubaliana kabisa na mdau hapo juu. Cherehani ni makini na mfano hata kwangu mie. Mpe Mpe Cherehani. Pia MPE Iddi .

Anonymous said...

huyu ndiye mgombea wa ukweli. u got my vote

Anonymous said...

Huyu Bwana Cherehani mimi nina hakika na utendaji wake wa kazi na hasa ndiyo KATIBU wetu. Hapa sina hata haja ya kupiga debe, nadhani imefika wakati tukubali kwamba Katibu wa Jumuiya yetu tumempata.

Anonymous said...

Kwa kweli kitendo chako cha kuchukua fomu ya kugombea uongozi kimenipa matumaini kwamba sasa Jumuia yetu itaongozwa na Mtu tunayemwamini kuwa ni makini. Bila shaka yeyote Kura yangu umeipata. Tunategemea Mazuri kutoka kwako hasa kwa kuzingatia Elimu yako na ukaribu yako kwenye jamii.

Mdau wa Baltimore,MD. said...

Kiongozi mzuri huanzia nyumbani kwake,maendeleo ya family level huleta maendeleo ya community level then maendeleo ya national level and then maendeleo ya dunia nzima.Kwa hili Mr. Cherehani ni vivid example.

Anonymous said...

I don't know what else do we need guys. This dude is for real.

Anonymous said...

AISEE ,MZEE CHEREHANI ,HAHAHAHAH.SASA NAKUBALI KUWA WANAINGIA KWENYE UONGOZI WATU WA MAANA,WENYE UPEO MKUBWA KTK KUIONGOZA HII WASHINGTON DC.ASANTE SANA CHEREHANI.HUYU JAMAA NI KIONGOZI KWELI.KAMA MTAMUULIZA MASWALI SIKU HIYO MTAONA.TUMPE KURA YA NDIO NA PIA NAMKUBALI SANA BWANA IDD.NIMEFUATILIA SIKU NYINGI ANA CV KUBWA NA PIA JINZI ANAVYOONGEA.TUWAPENI KURA YA NDIO

Anonymous said...

Cherahani si mtu wa kubabaisha.unajua tulikuwa na viongozi wa ubabaishaji sana hapo zamani ,sasa Mungu ibariki huyu jamaa ni mtendaji hasa.Alafu nimeona bwana idd,pia anafaa kuwa kiongozi wetu.jamani tusifanya makosa safari hii,tuchagua viongozi watakao leta ushirikiano,umoja.KULA YANGU MMEPATA

Anonymous said...

Huyu cherehani ni msomi aliyejificha.afadhari umejitokeza.unazidi kubeba mabox sana.njoo tusidie,njoo uwe mfano na kuendelea.Unajua kuna watu smart hawataki kushiriki kutuongoza kwa kweli sasa nimeona viongozi wa nguvu.Kula yangu umepata na mr idd umepata.nimesikia maojiano yako ,wewe kweli unatama mbali na unajua mataizo ya watanzania,na utayatatua vipi.kwanza ni msomi .MUNGU IBARIKI DMV.JAMANI SASA TUAMKE ,Tuwapigie kura hawa jamaa.Tumechoka kuweka watu kwa kufuata mkumbo.Tunataka watu mahili sasa

Anonymous said...

DMV sasa tumepata wagombea wenye sifa na utendeji ,na sio wengine bali Cherehani na Mr idd.Nawashukuru.nilifikiri ndugu zangu mnataka kupiga box tu.njoeni mtusaidie kuijenga hii jumuia yetu yenye ufa mkubwa.Sasa umepata dawa

Anonymous said...

VOTE IDD, VOTE CHEREHANI

Anonymous said...

watanzania wacheni ujinga nai aliwambia kusoma ndio uongozi mzuri wacheni ujinga kusoma sio tija tena ni bora mfute ujinga kama huo

Anonymous said...

Mashikoro magenyi sasa kidedea cha moto Dc mambo kwelikweli,Bwana cherehani kumbe box lilikuwa limekuzidia nilijua ulisha rudi bongo Bwana kwa hiyo ulichungulia Deal likawa si Deal chapa kazi ongeza status yako watu walisha kusahau mzee wa deal aka mazabe lakini ilikuwa inafaa kwa kukusaidia

Anonymous said...

mtajuta nawaambia! hizi comment zote ni za cherehani mwenyewe, huyu mtu ni selfish na majivuno. si kiongozi tunaemtaka huyu. fikiri kabla ya kutenda

Anonymous said...

HUYU NI MTU KARUKIA UONGOZI KAMA ALIVYOSEMA SIO ALIJIANDAA SASA AMEKUJA KWA NIA GANI KAPELEKA FORM DAKIKA ZA MWISHO

Anonymous said...

watanzania DMV jamani tujaribu kubadiriki huu sio muda wa kuanza kupigana majungu au vijembe, bali muda wa kutafakari nani ni kiingozi anafaa ktk jumuiya ya wana DMV,kwasababu mwisho wa siku nyie ndiyo muta hathirika endapo ntamchagua kiongozi ambaye hafai..mfano wewe mdau wa hapo juu unayeandika hizi ni comment za cherahani mwenyewe .sasa nikikuuliza swali umejuaje kama Mr chrahani amejitumia comment je unaushaidi?Mdau mwezangu ni vizuri ukawa unajitaidi kujenga na sio kubomoa.
NAWATAKIA UCHAGUZI MWEMA WANA DMV.
MWANAVIJIMAMBO-DRESDEN-GERMANY.

Anonymous said...

Wewe usituletee upumbavu hapa,kusoma ni kipimo cha kuongezwa cheo kazini hapa Tanzania na duniani kote.Kwa nini walioogopa umande hawapewi vyeo vya juu kwenye kampuni ?

Anonymous said...

HIVI WEWE UNASIKIA KWA MASIKIO AU MASABURI ? AMESEMA,ALIOMBWA NA MARAFIKI,WAZEE NA WATU MBALIMBALI KUGOMBEA HII NAFASI.MSONYOOOOO.KASIKILIZE TENA HALAFU UJE.