Hatua hiyo inatokana na polisi kukamilisha kazi ya kumhoji bosi huyo na mashahidi wengine na kisha jalada kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ambaye baada kumaliza kulipitia amelirudisha polisi ili taratibu za kwenda mahakamani ziendelee.
Bosi huyo, Emma Donavan, ambaye ni Meneja wa Wafanyakazi wa Ndani ya Ndege, atakayefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, anatuhumiwa kutoa lugha ya matusi kwa mfanyakazi mwenzake, Samson Itembe. Wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Deusdedit Kato, alisema walimaliza kumhoji Emma na jalada walilipeleka kwa DPP.
Habari kutoka Kituo cha Polisi cha Mamlaka ya Viwanja wa Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mwishoni mwa wiki, zilisema polisi walikuwa na kazi ya kukusanya ushahidi kutoka kwa wafanyakazi wengine kabla ya jalada kupelekwa kwa DPP.
Meneja huyo ambaye ni raia wa Uingereza, alikamatwa wiki iliyopita baada ya kusakwa kwa siku kadhaa.
Polisi walianza kumsaka Emma kwa madai ya kumtolea lugha ya matusi mfanyakazi mwenzake Itembe.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment