Arusha. Utata umegubika mazishi ya Wakili maarufu nchini, Nyaga Mawalla baada ya wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Fatma Karume kuwasilisha wasia wa marehemu kwa wazazi wake ambao alitaka azikwe kwenye shamba lake la Momela, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.
Hata hivyo, wasia huo unadaiwa kupingwa vikali na baba mzazi wa marehemu, Juma Mawalla huku akitoa sharti la kutohudhuria mazishi ya mwanaye iwapo akizikwa sehemu tofauti na Kijiji cha Marangu.
Mawalla, alifariki hivi karibuni baada ya kujirusha kutoka ghorofani akiwa Nairobi, Kenya alipokwenda kutibiwa.
Taarifa za awali zinasema kwamba Mawalla aliamua kujiua kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo, inadaiwa enzi zake za uhai alikuwa na uhusiano mbaya na baba yake.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka kwa mmoja wa mawakili wa kujitegemea mjini hapa, siku chache baada ya kifo cha wakili huyo, Karume alifika Kilimanjaro kuwasilisha wasia alioucha marehemu.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka kwa mmoja wa mawakili wa kujitegemea mjini hapa, siku chache baada ya kifo cha wakili huyo, Karume alifika Kilimanjaro kuwasilisha wasia alioucha marehemu.
Ilidaiwa binti huyo ambaye anatajwa kuwa karibu na marehemu enzi za uhai wake, alikutana na baba yake mzazi na kuusoma.
Hata hivyo, chanzo hicho kilidai kuwa pendekezo hilo la marehemu lilipingwa vikali na baba yake na kusema iwapo mtoto wake atazikwa Momela, hatahudhuria mazishi hayo.
Imeelezwa kipindi cha miaka miwili, wakili huyo hakuweza kuongea na baba yake hadi alipofariki, kutokana na uhusiano mbaya waliokuwa nao.
Imeelezwa kipindi cha miaka miwili, wakili huyo hakuweza kuongea na baba yake hadi alipofariki, kutokana na uhusiano mbaya waliokuwa nao.
Hata hivyo, wakili huyo alisisitiza kuwa, chanzo cha uhusiano mbaya baina yao ni kutokana na mzee Mawalla kumwonya mwanaye kuhusu biashara anazofanya baada kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa watu, maofisa usalama na baadhi ya polisi nchini waliokuwa wakifika kijijini mara kwa mara kumsemea. Mmoja wa mawakili wa Kampuni ya Mawalla Advocates, Lemy Bartholomew alipoulizwa kwa njia ya simu na gazeti hili kuhusiana na taratibu za mazishi, alisema ni mapema kuzungumzia suala hilo kwa sababu kuna vikao vya familia vinaendelea.
Wakili huyo alisema baada ya vikao hivyo, ndipo uamuzi utakapojulikana iwapo atapozikwa shambani kwake au nyumbani kwao kijijini Marangu.
Imeandikwa na Moses Mashalla na Peter Saramba .
Mwananchi
No comments:
Post a Comment