ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 7, 2013

JINSI YA KUFANYA UNAPOFELI MITIHANI

Inaelezwa kuwa kipindi cha kati ya mwezi mmoja na miwili baada ya matokeo kutolewa huwa ni hatari kwa uharibifu wa akili za wanafunzi waliofeli.

Wengi kati ya wanafunzi waliofeli huanza kuharibika kitabia muda mfupi baada ya kupoteza matumaini kutoka katika masomo yao. Uchunguzi unaonyesha vijana wengi huingia vijiweni na kuanza utumiaji wa dawa za kulevya muda mfupi baada ya kushindwa kuendelea na masomo. Msingi mkubwa wa mabadiliko hayo ya tabia huwa ni kuvunjika moyo na kupoteza dira ya kimaisha.
Inashauriwa kuwa baada ya kumalizika kwa mapumziko ambayo nimeyataja, wazazi na wanafunzi waliofeli wanashauriwa kufikiria hatua za kufuata kwa kutafakari uwezo wao kwa ujumla na kujadiliana kwa pamoja kama wanaweza kusonga mbele au hawataweza.
Inaaminika kwamba maamuzi yatakayofikiwa katika majadiliano yanaweza kuwa na tija tofauti na kufanya mipango mapema wakati akili za mwanafunzi na wazazi zinapokuwa zimechoshwa na majibu mabaya ya mitihani.


KUTOKUBALI MABADILIKO YA HARAKA

Jambo jingine la muhimu kwa wanafunzi waliofeli ni kutokubali kubadili tabia zao kwa kuiga haraka makundi ya vijana walioko mitaani. Mara nyingi mabadiliko hayo hutokana na matumizi mabaya ya muda unaokuwepo ambao awali wanafunzi husika walikuwa wanautumia kwa masomo.
Muda wa ziada unapotumika vibaya kwa kukaa vijiweni huweza kuathiri tabia na kupoteza mwelekeo wa kukabiliana na changamoto zinazokuwepo wakati huo za kutafuta shule na kusahihisha makosa.
Mara nyingi wanafunzi wanaomaliza hasa wa kike wanapokubali kuiga tabia za wenzao waliopo mitaani kwa kuungana nao katika matembezi na harakati za ujana huweza kuwasababishia mimba, magonjwa ya zinaa, kupoteza imani kwa walezi na wazazi hivyo kuweka mazingira magumu ya kusaidiwa.
Hivyo basi, mwanafunzi anapomaliza shule anatakiwa aoneshe utii kwa wazazi wake na jamii iliyomzunguka sambamba na kuonesha namna anavyopenda kusoma kwa kutumia muda wake kusoma vitabu, magazeti na kujielimisha mwenyewe. Kufanya hivi kuna faida nyingi, kubwa kuliko zote ni kupendwa na wazazi na hivyo kuwashawishi wamsaidie kivitendo kusonga mbele.
Lakini kama mwanafunzi anajifanya ‘msela’ wa kijiweni, akaanza uhuni na uvutaji bangi hawezi kuwa na nafasi ya kuendelezwa kimasomo na hata kama wazazi wataamua kumsaidia atafeli tena, kwa sababu hakutumia muda wake kujisahihisha makosa yaliyomfelisha mara ya kwanza.

KUFANYA UTAFITI
Mwanafunzi anapofeli na kurudi nyumbani na kukaa kwa kipindi alichoshauriwa anatakiwa aanze kufanya utafiti wa jinsi gani anaweza kujiendeleza kupitia kwa rafiki zake.
Kwa mfano awaulize wenzake waliomtangulia walifanya nini wakaendelea na masomo yao baada ya kufeli, awashirikishe waalimu wake kuhusu njia za kufuata baada ya matokeo kuwa mabaya na mwisho arudi kwa wazazi wake na kuwaletea majibu ya utafiti wake.
Hii itawasaidia wazazi ambao hawana mwamko wa elimu kupata njia sahihi za kumsaidia. Lakini pia yeye mwenyewe atakuwa na amani ya maisha mapya, jambo litakalomfanya ajiandae kuelekea hatua inayofuata.

GPL

No comments: