ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 16, 2013

KANISA LA SABATO DUNIANI WAPIMA UKIMWI NA KUCHANGIA DAMU HOSPITAL


 Katibu mkuu msaidi wa chama cha soko mkoa wa Morogoro[MRFA] Emmanuel Kimbawala akipima ngoma leo mchana.


lkumbukwe Kimbawala kabla ya kutimkia kwenye soka alikuwa ni mchungaji kiongozi wa kanisani hilo ambaye baada ya kuibuka mizengwe ya hapa na pale aliradhimika kujiudhuru kwa radhimia.


 Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakipima ngoma nje ya ofisi za Red Closs mkoa wa Morogoron leo


                                           Makao makuu ya kanisa hilo kanda ya mashariki


                                 Mchungaji wa kanisa hilo akipima ukimwi leo mchana

 Mchungaji kiongozi wa kanisani Hilo Bw  Toto Ndege Bwire Kusaga akihojiwa na mwandishi wa Mtandao huu muda mfupi baada ya kutoa damu.

                           NA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO
UMOJA wa vijana wa kanisa la Wasabato duniani kote leo wamepima  kwa hiyali gonjwa la UKIMWI kwa lengo la kuchangia damu  safi kwenye mahabara za hospital za maeneo yao .


Zoezi hilo limenywa duniani kote baada ya waumini hao kutoka kwenye ibada ambapo kwa dhehebu hilo la sabato siku yao ya ibada ni kila jumamosi

Kwa upande wa umoja wa vijana wa kanisa hilo  mkoani Morogoro nchini Tanzania baada ya kutoka kwenye ibada  wakiongozwa na mchungaji wao Bw Toto Ndege Bwire Kusaga  vijana hao walifulika kwenye makao makuu ya kanisa hilo kanda ya Mashariki yaliopo kata ya Sultani mkoani hapa na ofisi za Msalaba mwekundu wakigombea kuchangia damu kwenye mahabara za hospital ya mkoa wa Morogoro.

Akizungumza na Mtandao huu Mkuu wa ldara ya Umoja wa Vijana wa kanisani hilo mkoa wa Morogoro  Bw Samuel Muze Mgonja  alisema  huo ni mpango wa umoja wa vijana wa kanisa hilo duniani kote kuchangia damu kwenye   mahabara ya mahospital.

Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa kanisa hilo kanda ya Mashariki Mchungaji Sanga alisema


"Kila juma moja la mwezi wa tatu umoja wa vijana wa kanisa letu duniani kote hufanya matendo ya huduma ikiwemo hili la kuchangia damu kwenye mahabara za mahospital,ukisoma Mathayo 25  yesu alituagiza tuwahudumie wagonjwa"alisema Mchungaji huyo ambaye aliwasapoti vijana hao kwa kutoa damu kwenye ofisi ya makao makuu ya kanisa hilo.

Mbali na kuchangia damu hizo wafuasi hao wa kanisa la Wasabato walitakiwa kupima Ukimwi ambapo wale wenye damu safi ndio itaingizwa kwenye mahabara ya hospital hizo na wale wenye damu chafu itamwagwa na kwamba kwa mtu yoyote aliyehitaji majibu ya damu yake alitakiwa kufika kwenye ofisi hizo za msalaba mwekundu baada ya wiki moja

Mmoja wa wahudumu wa  Red Closs Bw Calvin Makula alipoulizwa ni kwanini majibu ya wapendwa hao yanachelewa kiasi hicho wakati kawaida ya vipimo hivyo ni muda wa kakribani robo  saa alijibu kwa mkatao" mimi sio msemaji wa Red Closs" 


Kigogo wa Red Closs mkoa wa Morogoro aliyefahamika kwa jina moja la Wille alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo naye alijibu kwa mkato" tuko bize sana  kama vipi njoo kesho tutapata muda mzuri wakujibu maswari yako"

No comments: