Wanariadha kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Wakenya walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph alebeba Medali ya Dhahabu.
Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.
Aidha katika mbio za Kilometa 21, Kenya ilitamba tena kwa upande wa wanaume baada ya wakimbiaji wake watatu kushika nafasi za juu ambapo Mshindi alikuwa ni Silah Limo huku nafasi ya pili ikienda kwa Bernard Kiprotich na nafasi ya tatu ikienda kwa Charles Ogari.
Mtanzania Dickson Marwa alinyakua nafasi ya nne na nafasi za tano na sita zikenda Tena Kenya kwa wakimbiaji Peter Kusgei na Evans Taigey nafasi ya saba ilishikwa na Mtanzania Stephano Huche na kuporwa tena na Kenya nafasi ya nane iliyoenda kwa Patrick Wambugu aliyekimbia mbele ya watanzania wawili waliofunga hesabu ya wakimbiaji kumi bora ambapo namba tisa alikuwa Said Makula na kumi alikuwa Peter Sule.
Shangwe ya watanzania iliibuliwa na Mwana dada Sara Makera Ramadhan baada ya kunyakua medali ya dhahabu kwa kuibuka mshindi wa kwanza mbele ya mkenya Vicomi Chepkemoi huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mtanzania mwingine Failuna Makanga.
Nafasi ya nne ilienda kwa Joyce Kiplimo wa Kenya aliyefuatiwa na mwenzake Pauline Muchiri kasha Mtanzania Catherine Tuku alishika nafasi ya sita na zilizosalia hadi nafasi ya kumi zikienda kwa Nchi ya Kenya ambao ni Nancy Kotch, Jacinta Mboani, Florence Cheruiyot na Phylas Jelagat.
Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.
Wakimbiaji wa Kenya wakipongezana baada ya kufanya vizuri katika mbio
Mfukuza Upepo kutoka Nchini Kenya na Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika Mbio za Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Eunice Muchiri akikimbia na kumaliza wapili mbio za Kilimeta 42 Wanawake, katika Mbio za Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Hakika mbio si kitu lelema, hapa ni Eunice Muchiri akitaapika baada ya kumaliza mbio hizo.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akimaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio za nyika za Kilimanjaro 2013. Poulsen amedhihirisha kuwa ni mwanamichezo na kuwa kocha wa Kwanza wa Timu ya Taifa kushiriki mbio hizo tangu kuanzishwa kwake miaka 10 iliyopita.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akisalimia mashabiki waliokuwa wakimshangilia baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio za nyika za Kilimanjaro 2013.
Wakimbiaji wa mbio fupi za nyika za Kilimanjaro waliopo chini ya udhamini wa Kampuni ya CFAO ya jijini Dar es Salaam wakichuana kumaliza mbio hizo.
Mbio hizi wapo waliokuwa wanazungukwa kama hapa wanavyopishana njiani. Kulia wakienda huku Kushoto wakirudi kumaliza.
CFAO walihakikisha maji na vipozeo vyote vinapatikana katika point ya Mweka
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akikimbia mbio hizo za kilometa 21.
Wadau Chris Magori kutoka NSSF na Swahiba wake nao walikimbia Kilometa 21.
Mdau Dominic Mosha akifurahi na kuonesha kuwa bado ananguvu ya kumaliza mbio za Kilometa 21.
Mkongwe wa Mbio za nyika akikimbia Kilometa 21. Babu huyu alimaliza mbio hizo.
Picha kwa hisani ya father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment