Shahidi wa utetezi katika kesi inayowakabili watu 54 ya kufanya maandamano isivyo halali, amedai mahakamani kuwa hajui kesi inayowakabili wala kama kuna masheikh wameshtakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Shahidi huyo wa 14 wa upande wa utetezi, Ramadhani Fadhil, alidai kwamba siku ya tukio alikuwa kwenye biashara zake na hakujua lolote kuhusu Waislamu pamoja na kuwa ni mfuasi wa dini hiyo.
Hata hivyo, alida kuwa alishangaa kuona askari wakimkamata na kumpeleka kituo cha polisi.
Alitoa ushahidi huo jana mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo.
Washtakiwa wengine wa upande huo wa utetezi walidai kwa nyakati tofauti kuwa hawakuandamana na hawakuwa na taarifa zozote za maandamano hayo.
Wakili wa utetezi, Hamidu Ubaidi, aliwaongoza washtakiwa hao kwa nyakati tofauti ambao pia walidai kuwa hawafahamu Sheikh Issa Ponda Issa, wala hawafahamu kesi yoyote inayowahusu masheikh inayoendelea mahakamani hapo.
Mshtakiwa Abubakar Bakari, alidai kuwa siku ya tukio alikuwa anaelekea Kariakoo kununua mbolea ya shamba lake na baadaye alikwenda Posta kuchukua fomu ya kuunganisha umeme katika nyumba yake iliyoko Vingunguti.
Hata hivyo, alidai kuwa alishangaa pale polisi walipomfuata na kumkamata.
Mshtakiwa mwingine, Abdallah Salum, alidai kuwa siku ya tukio, alikwenda kufanya biashara yake ya maji eneo la Mburahati na pasipo kufahamu lolote, alishangaa kuona askari wakimkamata kwa vile alikuwa amevaa kanzu na kofia.
Kesi hiyo itaendelea leo kwa kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment