Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana Kinjekitile.(picha na freddy Maro)
Dar es Salaam. Mshauri wa zamani wa Rais wa Mambo ya Siasa, Kingunge Ngombale Mwiru amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kujisikia vibaya jana.
Hata hivyo, haikuweza kubainika jana kuwa alipatwa na nini lakini ilifahamika kuwa jopo la madaktari bingwa lilikuwa likimfanyia uchunguzi ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.
Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa watu waliokwenda kumjulia hali Kingunge aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa wa dharura katika hospitali hiyo jana.
Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa watu waliokwenda kumjulia hali Kingunge aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa wa dharura katika hospitali hiyo jana.
Katika hosipitali hiyo, pia walikuwapo Mke wa Mzee Kingunge na mtoto wake, Kinjekitile.
Kingunge aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali za awamu zote nne, alikuwa akitumika katika masual mbalimbali muhimu ya kitaifa pamoja na kutoa ushauri kwa masuala ya uchumi na siasa kabla ya kustaafu.

No comments:
Post a Comment