ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 9, 2013

KIPA BRAZIL AFUNGWA MIAKA 22 KWA KUMUUA MPENZI WAKE NA KUWAPA MBWA WAILE NYAMA YAKE

Kipa maarufu wa zamani wa Flamengo ya Brazil, Bruno amehukumiwa kifungo cha miaka zaidi ya 22 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake wa zamani.
Katika hukumu iliyotolewa jana na jaji Marixa Fabiane Lopes Rodrigues, kipa huyo alipatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia Eliza Samudio aliyekuwa mwanamitindo maarufu.
Bruno alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake huyo wa zamani ambaye mwili wake haukuwahi kupatikana na kuna hofu huenda mwili huo ulikatwa vipande ambavyo walipewa mbwa kama chakula.
Pamoja na hivyo, ilielezwa Bruno alimshikiliwa mateka mtoto wao mdogo aliyezaa na mwanamitindo huyo.
Taarifa za kukamatwa kwake zimetawala vyombo vya habari vya Brazil na hiyo imekuwa hukumu ya pili amekumbana nayo Bruno, kwani tayari alishahukumiwa miaka minne na miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kumteka mwanamke huyo na kumtaka atoe mimba.
(Habari kwa hisani ya Salehjembe blogspot)

No comments: