ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 15, 2013

MGAHAWA WA KILIMANJARO MAMBO MSWANO

 Mgahawa wa Kilimanjaro uliopo 2310 Price Ave,, Silver pring, MD maeneo ya Wheaton umeanza kwa kishindo kwa Watanzania kumsapoti Mtanzania mwenzao wakiongozwa na Kaimu Balozi Mama Lily Munanka
 Asilimia 99.9 walikua ni Watanzania waliofika siku ya kwanza ya ufunguzi wa Mgahawa wa Kilimanjaro uliopo Wheaton, Silver Spring, Maryland.
 Kaimu Balozi Mama Lily Munanka akisalimiana na Majida Gao huku baba mwenye nyumba wake Arthur Gao akiangalia
Kaimu Balozi Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akisalimiana na watoto na wajukuu wa Balozi Nyang'anyi mara alipoingia kwenye mgahawa wa Kilimanjaro ambao umefunguliwa leo rasmi

Kaimu Balozi Mama Lily Munanka akiagiza chakula huku Afisa Ubalozi Abbas Missana akisubili zamu yake.

Kaimu Balozi Mama Lily Munanka katika picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi Abbas Missana (shoto), Suleiman Saleh (aliyesimama) na Mama Love Maganga
 Watanzania waliofika kusapoti Mtanzania mwenzao kwenye ufunguzi wa Mgahawa wa Kilimamnjaro uliopo Wheaton, Silver Spring, Maryland.

Watanzania wakimsapoti Mtanzania mwenzao kwenye mgahawa mpya uliofunguliwa leo Ijumaa March 15, 2310 maeneo ya Wheaton, Silver Spring, Maryland.

Watanzania waliofika Mgahawa wa Kilimanjaro kumsapoti Mtanzania mwenzao kwenye ufunguzi wa mgahawa huo uliofanyika leo Ijumaa March 15, 2013

 Watanzania wakiangalia orodha ya vyakula vilivyopo tayari kwa kuagiza
kwa picha zaidi bofya read more



4 comments:

Anonymous said...

Hongera sana ndugu yangu! Hii inatia moyo kwa kweli!Kila lakheri na baraka zote za mwenyezi mungu!...

baraka daudi said...

dmk,vizuri sana sasa na sisi watanzania tuna restaurant yetu ya kujivunia,nimefurahi sana kuona hii habari."big up bro"we will support you 110%,na sisi wapenzi wa uji wa iliki usitusahau!!!! HONGERA SANAAAAAA

Anonymous said...

mambo ya maendeleo haya hongera wandugu ushauri kidogo wateja wako umelenga wabongo tu? nakushauri tangaza na kwa wenyeji wamarekani na mataifa mengine

Anonymous said...

kweli sasa watanzania tunaonyesha ni jinsi gani sasa tunaupendo! haya ndo maendeleo jamani, kusupportiana hilo ndilo jambo la maana, tuweke majungu kando! hakika tutafika mbali!ili mradi tufungue biashara zinazotofautiana! sio leo hii mwenzetu kafungua mgahawa na wewe kesho unafungua mgahawa sehemu hiyo hiyo! hapo ni kuleta mgawanyiko!BIG UP uliyefungua mgahawa!