ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 21, 2013

MSTAHIKI JERRY SILAA ATAKA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA ELIMU KATIKA MANISPAA YA ILALA.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika Shule ya Msingi Kigilagila iliyopo maeneo ya Gongo la Mboto kama mgeni rasmi katika hafla fupi iliyoandiliwa na mfuko wa Pensheni wa PPF ya kukabidhi vitabu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akitambulishwa kwa Meneja wa Penesheni Bi. Chevu Sepeku( kushoto) mara baada ya kuwasili katika shule hiyo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba na Wa pili kulia ni Afisa Uhusiano wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiteta jambo na mmoja wa wanakikundi cha kwaya cha shule hiyo mara baada ya kuwasili.
Kwaya ya Shule ya Msingi Kigilagila ikipiga wimbo wa Taifa kuashiria kuanza kwa hafla hiyo.
kwa picha zaidi bofya

Meza kuu wakiupa heshima wimbo wa Taifa: Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa (wa pili kushoto), Meneja wa Penesheni Bi. Chevu Sepeku( kulia) , Wa pili kulia ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kigilagila Verian Mfugale.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kigilagila Verian Mfugale akiukaribisha ugeni katika shule hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za vitabu shuleni hapo pamoja na kwa watoto wawili yatima ambao wazazi wao walikuwa ni wanachama wa mfuko wa Pensheni wa PPF na kuendelea kusomeshwa kupitia FAO LA ELIMU linatolewa na mfuko wa Penesheni wa PFF.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza jambo na Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu iliyoenda sambamba na Kampeni ya Kutangaza FAO LA ELIMU.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya Kigilagila na kufafanua kuwa mambo yanayofanywa na Mfuko waPensheni wa PPF katika kurekebisha baadhi ya mafao yake haswa fao la kifo, si tu yatasaidia kuwapa elimu wanafunzi wanaoguswa bali yatatia mkono katika kuboresha elimu katika mfumo mzima wa taifa letu na moja kwa moja katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.
Aidha Mh. Silaa ametoa wito kwa watanzania akisema kwa kuwa sasa mifuko hii ya pensheni imefungua milango, sio kwa watu walioajiriwa pekee ndio wanaopaswa kujiunga na mifuko hii ya pensheni, lakini hata kwa watu waliojiajiri, wakulima na hata wafugaji wana uwezo kabisa kisheria kujiunga na mifuko ya pensheni na kunufaika nayo.
Pia ameupongeza mfuko wa PPF kwa yale wanayoyafanya kwa watoto wa watu waliofariki wakiwa wanachama wa mfuko huo, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya wanafunzi 1, 333 wamelipiwa gharama mbalimbali zilizofikia jumla ya shilingi milioni 682.9 kitu ambacho ni jambo la kupigiwa mfano.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba akielezea nia ya kutembelea shule hiyo ni kutoa msaada wa vitabu kwa sababu tunaamini kwamba vitabu tutakavyo vitoa vitawasaidia wanafunzi waliopo hapa kuweza kupata elimu nzuri na kufanya vizuri katika mitihani yao na vilevile hawa ndio viongozi wa baadae. Vilevile katika hii shule ya Kigilagila sisi kama PPF tuna wanafunzi ambao tunawasomesha hivyo sisi ni wadau wa shule hii na tunatumia fursa hii kuwashauri waalimu na pia wazazi kujiunga na mfuko huu kwa manufaa ya baadae.
Meneja wa Penesheni PPF Bi. Chevu Sepeku akitoa elimu kwa wageni na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo kuhusiana na taratibu za utoaji wa mafao ya Elimu na kufafanua kuwa hutolewa ili kugharamia sehemu au gharama zote zinazohitajika katika elimu ya mtoto wa mwanachama aliyefariki ambapo gharama hizo ni kuanzia elimu ya chekechea hadi kidato cha nne.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi zawadi kwa mtoto wa darasa la Saba Ummy Abdalah kwa niaba ya wanafunzi wenzake. Ummy Abdalah ni miongoni mwa wanafunzi wanaosomeshwa na PPF kutumia FAO LA ELIMU baada ya wazazi waliokuwa wananchama wa mfuko huu kufariki dunia.
Mtoto Shakila Abdalah wa darasa la pili naye akipokea zawadi kutoka kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Veriana Mfugale akishihudia tukio hilo. Kwa picha zaidi bofya hapa

No comments: