ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 16, 2013

MWANA FA AITAKA SERIKALI IRUDISHE MFUMO WA ANALOGIA

Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa mfumo wa digitali unawaumiza.
Akiongea na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye ving’amuzi.
“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.
Alisisitiza kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.

1 comment:

Anonymous said...

Bongo hovyoo sana...wbuni wametumia hio mifumo yote miwili hadi huo wa digitali ulipoenea sehemu zote ndo wakauondoa kabisa mfumo wa analogue...viongozi wetu cjui huwa akili wanafikiria toka wapi utasema mat*&^&&* banaa.