ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 15, 2013

Mwanaharakati akimbia vitisho vya kuuawa



Dar es salaam. Mwanaharakati Albanie Marcossy, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Civil and Political Right Watch (CPW) ameondoka nyumbani kwake Kimara Dar es Slaam akidai kilichomwondoa ni kupokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.

Marcossy, awali aliwahi kufanya kazi kwenye Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) ambako alikuwa mmoja wa waliopeleka mashtaka kwenye Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Septemba 28, 2012 dhidi ya serikali kutokana na mauaji yenye utata ya watu 23 akiwamo Mwandishi wa habari Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Akizungumza jana kutoka alikokimbilia, Marcossy alisema ameamua kuikimbia nyumba yake kwa ajili ya usalama na kubainisha kuwa taarifa ya vitisho vyake aliwasilisha kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD-Coalition,) Onesmo Olengurumwa.

Olengurumwa alithibitisha kupokea taarifa hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alipoulizwa jana alisema polisi hawana taarifa kuhusiana na kutoweka kwa mwanaharakati huyo wala kutishiwa kutokana na kutopokea taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo .

No comments: