ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 15, 2013

MKULIMA ATUMIA USAFIRI WA BAISKEL KUMSAFIRISHA MTOTO WAKE MGONJWA UMBALI WA KILOMETA 10

WAKATI baadhi ya viongozi na watu wenye uwezo kifedha wanapoumwa hata kama ni mafua hukimbilia nje ya nchi kwa matibabu,hali kama hiyo imekuwa tofauti kwa watu mafukala ambapo hivi karibuni Mkazi mmoja wa kijiji cha Kiloka Wilaya ya Morogoro vijijini Mohamed Juma alinaswa kwenye msitu mnene akimkimbiza hospital mtoto wake kwa kutuma usafiri wa baiskel huku akiwa amemfunga kwente tenga la nyanya

Mwandishi wa habari hizi ambaye hufanya ziara za kusaka matukio ya kijamii kwenye vijiji mbali mbali vya mji wa morogoro,alimnasa mzee huyo kwenye msitu huo akinyonga kwa kasi baiskeli hiyo kwa lengo la kumuahisha kwenye zahanati ya kijiji hicho.
Aliposimamishwa na kuhojiwa mzee Juma alisema mtoto wake huyo Athuman Mohamed[5] alikuwa akisumbulia na ugonjwa wa Malaria,hivyo alimua kumpela kwenye Zahanati hiyo aliyodai iko umbali wa takribani kilometa 10 kwa kutumia usafiri huo wa baiskeli.

" Jana usiku hatukulala amejiwa na homa kali hivyo kutokana na umbali wa safari niliamu kumsafirisha kwa kumuweka kwenye tenga ninalotumia kuvunia vyavya shambani, mbali na umri wake mdogo pia alikuwa akitetemeka sana kwa homa kali hivyo kama angeketi kwenye kiti cha baiskeli usalama ungekuwa mdogo, mama yake alishauli nimfunge kwenye tenge"alisema mzee Jumaa

Alipoulizwa kama anafedha za matibabu alidai kwamba ameradhimika kuuza kuku wa kiume 'Jongoo' kwa wauza Chips kwa lengo la kupata ujira wa kumtibu mtoto wake.mwandishi wa habari wa Mtandao huu alimuongezea kiasia flani cha fedha ili kimsadia kwenye matibabu hayo
SOURCE DUSTAN SHEKIDELE

2 comments:

Anonymous said...

Wana DMV wenzangu, pamoja na kukaa huku mamtoni, tusisahau kule tulikotoka. Watu wana hali mbaya sana nyumbani. Huko ndiko tulikotoka. Hata kama ni kubaya kiasi gani, nyumbani ni nyumbani.

Anonymous said...

Wenyewe wanakwambia bongo tambarare..bongo New York!!! wanasahau kwamba Tanzania c Dar Es Salaam peke yake..
mdau wa london