ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 30, 2013

'Nisaidieni kuokoa maisha ya mwanangu'

Selemani Abdallah

Hana sehemu ya kutolea haja kubwa
Selemani Abdallah (pichani), amezaliwa bila sehemu ya kutolea haja kubwa hali iliyosababisha kujisaidia kupitia mdomoni.

Kutokana na tatizo hilo, Veronica  Laurent (26), mzazi wa mtoto Selemani anaomba msaada wa matibabu na chakula kuokoa maisha ya mwanae.

Aliwaomba watakaoguswa na  tatizo hilo kumchangia  Sh milioni mbili kwa  ajili ya matibabu na huduma muhimu.


Selemani anahitaji kufanyiwa upasuaji kumtengenezea  sehemu ya kutolea haja kubwa kutokana na kasoro za kuzaliwa.

Veronica anayeishi Bunju Dar es Salaam, akizungumza na mwandishi wetu, alisema mwanae mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu alizaliwa Mwananyamala  hospitalini na kugundulika na tatizo hilo.

Kutokana  na kasoro hiyo, alifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutengeneza njia ya muda ya kutolea haja kubwa.

“Alitengenezewa njia ya muda tumboni karibu na kitovu ambapo palipasuliwa na kuuvuta utumbo nje ili kupitisha choo jambo ambalo lilifanywa kama huduma ya kwanza.” 
Aliongeza, “anatumia sehemu hiyo kutoa kinyesi , mkojo hutoka kwa njia ya kawaida lakini kinachomuumiza ni utumbo uliovutwa nje kuendelea kutoka muda wote na kusababisha kidonda kibichi.”

Alisema licha ya kidonda hicho kuwa kibichi  kinatoa damu na harufu na kwamba anaukandamiza utumbo ili kuurudisha ndani hali inayoongeza maumivu.

Alisema baba wa mtoto huyo alimtelekeza kutokana na kuzaa  mtoto mwenye kasoro, alitimuliwa kwa mwajiri aliyekuwa anafanyakazi za ndani kufuatia  tatizo la mwanae.
Veronica alisema anahitaji  zaidi ya Sh milioni 1,500,000 kwa ajili ya upasuaji pekee.

Veronica na Selemani  hawana makazi wanaishi kwenye viwanja vya Kanisa la Ufufuo na Uzima  lililoko Kawe na kuhudumiwa na waumini.

Aliomba watakaoguswa na tatizo lake wafikishe msaada kwa Mhariri wa Nipashe kwa simu  0714-654164 ama ufike  ofisi ya The Guardian Ltd Mikocheni karibu na kituo cha televisheni cha  ITV.

Kadhalika anaweza kuwasiliana na Veronica kupitia namba 0763-411777 au 0712-004677.
CHANZO: NIPASHE

No comments: