Vatican, City. Siku moja baada ya kuchaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ameanza kazi huku akitarajiwa kuteua wakuu mbalimbali watakaohudumu ndani ya Vatican chini ya uongozi wake.
Inatarajiwa kuwa, Papa Francis atateua wakuu watakaoleta mabadiliko makubwa katika uongozi na kubadilisha mwelekeo wa kanisa hilo, uliosukwasukwa na kashfa mbalimbali.
Mwishoni mwa wiki ijayo, Papa anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari katika mkutano maalumu, ambapo ataelezea namna atakavyojipanga kuendesha kazi zake za kuwaongoza waumini zaidi ya bilioni moja duniani.
Mwishoni mwa wiki ijayo, Papa anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari katika mkutano maalumu, ambapo ataelezea namna atakavyojipanga kuendesha kazi zake za kuwaongoza waumini zaidi ya bilioni moja duniani.
Jumapili ijayo, Papa Francis I, ataongoza misa yake ya kwanza akiwa kama Papa na siku ya Jumanne, atatawazwa rasmi kuwa Papa. Papa Francis I ni Kardinali wa kwanza kuchaguliwa kuwa Papa kutoka nje ya Bara la Ulaya kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, akichukua nafasi hiyo baada ya mtangulizi wake, Papa Benedict XVI kujiuzulu mapema Februari mwaka huu.
Mkosoaji wa Serikali yake na kipenzi cha maskini
Papa Francis I, anayetajwa kuwa karibu zaidi na maskini na wasiojiweza, pia ni kiongozi wa kwanza kutoka katika Shirika la Jesuit kuteuliwa kuwa Papa.
Licha ya kupendwa na waumini wake, Papa huyo mwenye umri wa miaka 76, amekuwa hana uhusiano mzuri na Serikali yake kwa sababu ya kuikosoa mara kwa mara. Mara kadhaa amekuwa akipingana na Rais wa Argentina, Christina Fernandez, katika masuala ya mapenzi ya jinsia moja na utoaji wa mimba.
Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki, Amerika Kusini ambapo kanisa hilo lina waumini wengi zaidi duniani, Kardinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa udhibiti wa kisiasa katika nchi zilizo Bara la Amerika Kusini. Inaelezwa kuwa Papa Francis I,
aliwaambia Raia wa Argentina kutotumia fedha nyingi kwenda nchini Italia kusherehekea kuchaguliwa kwake kuliongoza Kanisa Katoliki, badala yake aliwaasa wawape fedha hizo maskini. Hata alipopata uongozi wa juu wa kanisa mwaka 2001 nchini Argentina, hakukaa katika jumba la kifahari, bali aliishi katika nyumba yake ndogo.
Kwa miaka mingi amekuwa akitumia usafiri wa umma kwa safari zake za mjini, alijipikia mlo wake na alipenda kunywa chai ya asili ya watu wa Amerika ya Kusini. Papa Francis I aliyekuwa Kardinali wa Jimbo la Buenos Aires, inasemekana aliibuka nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005.
Papa Francis I, ambaye jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio, alizaliwa katika Jimbo la Buenos Aires, huko Argentina akiwa ni mtoto wa mfanyakazi wa reli. Alipokuwa mdogo, Papa Francis aliondolewa pafu moja baada ya kubainika kuwa na maradhi yaliyolishambulia pafu hilo.
Alisomea elimu ya Kemia na baadaye alipata shahada ya uzamivu na kuwa mhandisi, hata hivyo akiwa na umri wa miaka 21 tu, aliamua kusoma seminari na kuwa padri katika Shirika la Jesuit hadi alipoteuliwa kuwa askofu, kabla kuwa Kardinali na sasa Papa.
Kaimu Msemaji Vatican,Thomas Rosica alikaririwa akisema Papa, alichagua jina la Francis.
kwa kumuenzi Mtakatifu Francis wa Assisi, aliyekuwa kipenzi cha maskini.
Hata hivyo,Rosica alisisitiza kuwa Papa huyo si Francis wa kwanza, bali ni Francis tu, jina hilo litaweza kubadilika na kuwa Francis 1 pale tu atakapotokea Francis wa Pili.Papa Francis ni mmoja wa watoto watano wa wahamiaji wa Kitaliano nchini Argentina, mama yake akiitwa Regina Maria Sivori aliyekuwa mama wa nyumbani.
Mwananchi
1 comment:
Waandishi wa bongo achane ku copy and ku paste habari. Papa anakutana na waandishi wa habari ni kawaida kwa kila papa kukutana na waandishi wa habari kuwashukuru kwa kazi walizofanya wakati wa conclave...hawezi kuelezea chochote juu ya mpango wake...Canon Law hipo wazi kwa hili. Atakachokifanya saturday atawashukuru kwa kuripoti habari za conclave and kuwashukuru personally. Hizi siyo siasa...also kuhusu mabadiliko hawezi fanya hadi baada ya mwaka mmoja hiyo pia ni wazi ndani ya canon law.
Fr.Liundi
Rome -Italy
Post a Comment