ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 8, 2013

Sawa unampenda mkeo, kwa kipi hasa?

KWANZA namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya na ufahamu wa kuyasema machache kwa uwezo wake. Naendelea kumshukuru yeye kwa kile kidogo alichonipa kuwafikia watu na kuwa msaada na dira kwa wengi.

Ukweli kona hii imekuwa ikipata maswali mengi ambayo nimekuwa nikiyajibu kwa njia ya SMS au kwa kuzungumza moja kwa moja na mhusika. Kuna maswali ambayo yanaulizwa huku mhusika akiwa ameshatoa jibu bila kuelewa.

Kuna rafiki yangu mmoja amenitumia ujumbe ambao ni mzito kidogo, akihitaji msaada wangu wa kiushauri. Tumezoea kuona wanawake wengi wakiingizwa katika majaribu mazito ya kulazimishwa kuingiliwa kinyume na maumbile na wanaume huku wanaume hao wakijinadi wanawapenda.
Nilisema siku zote anayekupenda atakulinda, hawezi kukuomba kitu akijua kabisa mchezo ule ni mbaya na una madhara makubwa kwa mwenzake. Leo sitazungumzia madhara ya mwanamke au mwanaume anayependa mchezo huo mchafu ambao pia unapingwa
na dini zote.

Leo kuna kitu kingine nataka kukizungumza. Kuna mtu utakuta anafanyiwa vitu vya ajabu katika mapenzi ambavyo si sahihi lakini bado anajitoa mhanga ili kuokoa penzi lake.
Mfano, hivi karibuni rafiki yangu aliniomba ushauri kuwa mkewe ambaye yupo naye mwaka wa tatu sasa na wamebahatika kupata mtoto mmoja, anamlazimisha amuingilie kinyume cha maumbile na kama hataki ampe talaka yake.

Lakini baada ya kumbana alinieleza tabia ile mkewe aliianza Oktoba, mwaka jana, lakini kumbe wakati ananiuliza tayari kamridhia mkewe mara tatu.
Najiuliza mtu huyu alitaka kweli ushauri au nini! Kwa nini hakuuliza wakati mkewe ameanza tabia ile ili tumsaidie, lakini amemkubalia zaidi ya mara tatu kwa kisingizio anaokoa ndoa? Je, ni kweli ndoa inaokolewa vile? Nani anayehitaji ndoa kati yake na mkewe? Ni kigezo gani mwanamke anakuwa nacho kuhakikisha humpotezi?

Hapa inaonekana kabisa hakuna mapenzi bali kuna shinikizo la mapenzi, kama mwenzako anataka kitu ambacho hakiwezekani usiamini kuna mapenzi.
Unaona kabisa mwenzako hana mapenzi na wewe anakulazimisha kufanya mambo yasiyowezekana lakini unasema unampenda, kwa kipi hasa kinachokufanya uiharibu ndoa yako?

Huyo mkeo anajua madhara ya kuingiliwa kinyume na maumbile? Na huo mchezo kama haukuanza kwako kautoa wapi? Kwa akili ya kawaida kama mwanzo wa ndoa yenu hakuwa na tabia hiyo, huoni mwenzako si muaminifu kwa kuwa inaonekana aliutoa nje mchezo huo mchafu na kuuleta ndani?
Kwa nini mwanamke awe na jeuri ya kukulazimisha kufanya ujinga huo, kwa nini usimhoji? Hujioni kuwa wewe ni limbukeni wa mapenzi, mwanaume suruali usiye na kauli kwa mkeo!

Tabia hizi zipo ndani ya majumba yetu, hivi kama wewe mwanaume shababi, mkeo anaweza kukueleza kitu cha kipuuzi kama hicho nawe ukakitekeleza kwa vile tu unampenda! Si kwa tabia hiyo ya mwanamke kulazimisha kuingiliwa kinyume, ila ndani ya nyumba zetu kumekuwa na matatizo yanayowatesa watu kila kukicha.
Wapo wanawake wanaolazimisha maisha tofauti na kipato cha wenzao na akikosa anachotaka anaondoka au anadai talaka. Unajikuta una madeni kila kona kumfurahisha mkeo, ukiishiwa anakukimbia.
Unateseka, huna raha ya ndoa, unasema unampenda hutaki kumpoteza. Nauliza swali la awali, unampenda kwa kipi hasa? Kwa sura na umbile lake zuri? Mtu anayekupeleka kinyume na mipango yako hakufai, si mtu sahihi kwako kwa vile hana mapenzi nawe ila yupo nawe kwa ajili ya kukidhi haja zake.

Mkeo kaharibika, aibu utakayoipata mbele ya kadamnasi siku akiwa anajifungua, ndiyo utajua kama kweli ulikuwa unampenda au unalinda ndoa! Acha uzoba, hakuna mwanaume wa hivyo.

GLP

No comments: