ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 15, 2013

UCHAGUZI CCM DMV, WAINGIA DOA, WAOGOMBEA 6 WAJIENGUA

Wagombea sita wamejitoa katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa CCM DMV uchaguzi utakaofanyika kesho Jumamosi March 16, 2013 kwenye Address ya 500 Sligo Ave. kuanzia saa 9 alasili (3pm) ET.

waliojitoa kwenye uchaguzi huo ni Mrisho Mzese aliyekua anagombea nafasi ya Mwenyekiti, Al Amin Hassan Chande Othman aliyekua akigombea nafasi ya Mwenyekiti wa Vijana, Steven Ngosha aliyekua akigombea nafasi ya Katibu Mwenezi na Itikadi, Warashi Khamisi na Ismail Abubakar Mwlima waliokua wakigombea nafasi ya Halmashauri Kuu ya Tawi na Fadhili Londa aliyekua akigombea nafasi ya Katibu wa Vijana.

Sababu kubwa ya wagombea hao sita kujitoa ni kuwa na wasiwasi wa kupanga matokea na kujiunga kwao na CCM DMV na hatimae kugombea ni mapenzi yao na chama lakini wanaona matatizo tangia kwenye kamati ya uchaguzi mpaka kwenye uchaguzi wenyewe na kusema kuna wagombea wanaotakiwa kushinda na sio wao ndio maana tumeamua kujitoa.

Tangia uchaguzi huu utangazwe kumetokea wingi wa wanachama wapya waliotaka kujiunga na chama na wachunguzi wa mambo wanasema sababu ni kutaka kuuondoa uongozi wa muda  uliokuwepo madarakani lakini katika uchaguzi utakaofanyika hiyo kesho ni kiongozi mmoja tu aliyekua kwenye uongozi wa muda anayegombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama.

Vijimambo ilmpigia simu mmoja wa wanakamati ya uchaguzi kujua kulikoni nae alisema kujitoa kwa wagombea, habari hizo nae amezisikia mitaani wagombea hawajaiandikia barua kamati lakini cha msingi ni kwamba kunapotokea wagombea wawili ni lazima aibuke mshindi sasa kama wewe unaona utashindwa uchaguzi na kuamua kujitoa na bila kufuata taratibu na kuamua kupeleka taarifa kwenye vyombo vya habari kujitoa kwako basi kiongozi huyu anatatizo na kitu kingine Viongozi hawa waliojitoa walikua wanataka wapewe kadi za kuandikisha wanachama na taratibu za chama zilivyo wanachama wapya husajiliwa na uongozi na si mgombea.

21 comments:

Anonymous said...

Asiekubali kushindwa si mshindani, Kwa sababu ya kuogopa kushindwa mtu unaamua kujitoa sasa kilichokufanyeni mgombanie in the first place ni kipi? Hawa ndio waharibifu wa amani. Wengine mulikua na nafasi zenu peke yenu tayari mulikuwa mumeshinda. Kumetangazwa uchaguzi waliojitokeza ni wachache sio kila mtu anataka kuwa kiongozi, Sasa mlipojiandikisha mulikuwa hamuna malengo na dhamira nzuri na chama..Chama kinaundwa hata na wanachama kumi. Mimi ningekuwa mmoja wa wanakamati nisingekubali hawa wagombanie tena next time. Kama watoto vile mnatupa vinyonyo chini kisa hamjaambiwa mtashinda..

Anonymous said...

samahani luka mimi nauliza huku tanzania tumefuraishwa sana na kamati ya uchaguzi kama mwana ccm hauwezi kususia uchaguzi kama demokrasia inatendeka kesho wasingejitoa kabisa hii ni dalili ya kushindwa kabisa pole dmv

Anonymous said...

Tunashukuru kwa maelezo toka kwenye kamati ya uchaguzi. Hatahivyo wapo wagombea ambao wameshapewa kadi ili wakaandikishe wawachama wapya (kama sehemu ya kampeni zao) ambao ndiyo watakaowapigia kura. Majina yapo na kama nitapewa baraka na kamati ya uchaguzi, nipo tayari kuwataja pamoja na kadi namba zao. Kwanini baadhi ya wagombea waruhusiwe kuandikisha wanachama wapya na wengine wasiruhusiwe?

Anonymous said...

wana ccm wenzangu msikubali kuyumbwishwa na hao vijana. kwanza kabisa wameonyesha jinsi gani hawawezi kuongoza,wagombea gani wanaogopa uchaguzi. tunaomba tume iendelee na kazi nzuri wanayofanya. kesho wana ccm wote kwa pamoja na wingi tunaenda kuchagua viongozi wetu aibu iwashike mliojitoa kwa sababu ya agenda zenu za siri,ccm haina udini wala ukabila,msituletee mambo yenu ya udini ktk chama chetu. kidumu chama cha mapinduzi

Anonymous said...

hawa jamaa ni mamluki,wanakimbilia ktk vyombo vya habari badala kuja kwa wanachama kulalamika,kweli hawawezi kuongoza. inabidi waende mafunzo ya chama

Anonymous said...

Jamani hebu na tujiulize haya yote yametokana na nini na hawa wagombea wamefikaje kuamua uwamuzi mkubwa namna hii? Kwanza kabisa kama chama kiliweza kuchukua uwamuzi na ku-extend muda wa kurudisha form kwa wagombea kilishindwaje ku-extend muda wa huu uchaguzi? Na hapa ndipo walipokosea, huu ulikua ni wakati mzuri wa kuwahamasisha watu kujiunga na chama including mimi mwenyewe kadi za kujiunga zinatakiwa nyingi lakini wakuu wanabania na sababu ya kubania ni kwamba UCHAGUZI TAYARI UMESHAPITA, WANA DMV AMKENI kesho munaenda ku past time tu huu uchaguzi umeshapita kwasababu daftari la wapiga kura liko mikononi kwa wakuu na ishajulikana kura ngapi zitapigwa na wapi zitaenda sasa mukiomba mu-extend siku ya uchaguzi mutawaharibia hesabu na mipango yao. Watu hawathamini chama na maslahi ya chama bali wanathamini matumbo yao THIS IS DISGRACEFUL

Anonymous said...

mfa maji haishi kutapatapa,wana dmv wameamka ndio maana walichagua tume huru ya uchaguzi februari 24,2013 ili kusimamia uchaguzi. hao vijana walikuwa wanataka kupandikiza mamluki wao,wapi duniani uliona kadi za uanachama zinatolewa wiki ya uchaguzi kama sio mamluki.tawi limefunguliwa toka mwaka jana mlikuwa wapi msiwahamasishe watu wachukue kadi. mnajua kabisa hamwezi kuchaguliwa sababu ndio mnajitoa,kwa taarifa yenu dmv tumeamka nyinyi ndio bado mna mambo ya kuvuruga amani,aibu sana mnajitia katika jamii.

Anonymous said...

hivi jamani yeye huko marekani mbona mnatia aibu!! tulifikiri labda wenzetu mnaexposure mtakuwa na akili,hata katiba hamuijui eti tarehe uchaguzi isogezwe mbele kisa nini. tarehe za uchaguzi zinapangwa na mkutano mkuu wa wanachama. na nafikiri wanachama walikubaliana iwe machi 16,2013 tuliona katika blogu zenu za huko. sasa hawa mamluki wanasema kwa nini tume haikusogeza mbele muda!!. wanachama walifanya lini mkutano wa kuomba uchaguzi uongezwe mbele,hawa jamaa bora hata wamejitoa hawajui hata kanuni za chama. kaka luka wape hiyo tume ya uchaguzi salamu zetu waambie wanafanya kazi nzuri,wana msimamo hao ndio wangetkiwa kugombea sio hao wababaishaji waliojitoa. nendeni vyama vingine ccm haihitaji wanachama ambao hawajui nini maaana ya uchaguzi

Anonymous said...

uwiiii yaani nimecheka na hii haijawahi kutokea.. jamani ee kuvuja kwa pakacha furaha kwa mbebaji, mumesusa watu wala chama kilifunguliwa tokea mwaka jana mkapiga majungu mpaka, Sasa mnaogopa kushindwa mnasusa.Na hao wanaotaka kujiunga sasa ili wawapigie kura walikuwa wapi..Kama watoto vile. Sasa kama unaogopa mwanachama hai hawezi kukupa kura yake je ukileta fake atakusaidia nini. Mimi sijawahi kusikia watu wanajiunga na chama siku mbili kabla ya uchaguzi ili wapige kura tu. Na kama ni hivyo ina maana watu wa CCM tujiunge na CHADEMA siku ya kupiga kura ili tuwaharibie? Wewe unaogopa kushindwa kaa kimya au ulikuwa usijiandikishe mpaka una uhakika umejiandaa. Kwa kiiengreza hawa watu wanaitwa COWARDS. Si wana CCM kabisa na wala sio wajenga Nchi. Ni aibu kubwa kuitwa wana CCm.

Anonymous said...

Sasa hawa wakuu mbona wanawakimbia hawa waliojitoa? wamedai kwamba hawawezi kujitoa hivi hivi inabidi wafuate taratibu na inatakiwa signature zao....wanafanya hivo kwa maana ya kua wanajua bila ya wagombania hakuna uchaguzi...kwahiyo hawa waliojitoa majina yao yataendelea kuweko kesho kwasababu munatafutwa ili wafute majina yao munawakimbia...nyinyi uchaguzi mulishamchagua munayemtaka zamani tu kwahiyo musipoteze muda wetu kutuitisha kesho tunaenda kumpigia nani kura na wapinzani washajitoa?

Anonymous said...

Kama wameshajitoa watu Sita tayari, kesho tunaenda kumpigia nani kura??????

Anonymous said...

Yaani kuna mijitu sijui ikoje,eti unatishia nyau,haaahaaahaaaaa.hata mkijitoa haisaidii hamumkomoi yeyote yule,ni aibu kwenu mliojitoa,halafu eti mnataka kuwa viongozi wa ngazi za juu,sasa jazba hizo mnazotumia mitaani mnazani mnaweza kuongoza kweli???.Hata kama uchaguzi utakuja kuludiwa tayari nyinyi sasa ndio mmejitia doa,inajionyesha dhahili.

Anonymous said...

Mimi nilijua DMV CCM na watu wengine longolongo kwa ajili ya yule dada wa Kichaga,kumbe kuna matatizo ya wenyewe kwa wenyewe wanachama,hata kama akiingia yeyote yule itakua hivyohivyo tu.Dada wa watu amewaachia sasa game linawashinda mapemaaa

Anonymous said...

Eti unataka kadi semanini au mia,siku zote ulikua wapi???hao ndio mamluki wa chama ,chama kilianzishwa zamani mwaka jana,hukutokea hata siku mojaaaaaa for god sake,leo hii uchumie kivulini na unakuja na kundi lako chafu ambalo lilikua linatukana watu wa CCM kweli ni halali hiyo??kisa wakupigie kula,na tayari ushaonyesha wewe si kiongozi bora.Ndio yaleyale wananunua kadi kwa wingi akichaguliwa wamtakae wanarudisha kadi,nawapongeza sana tume ya uchaguzi.

Anonymous said...

VIVA TUME YA UCHAGUZIIIIIIIIII,nyinyi ni majabali,na tunataka watu strong kama ninyi.

Anonymous said...


LEO NAKUMBUKA USEMI WA BABA YANGU KUWA ELIMU NI KITU MUHIMU SANA KUWANACHO HAPA DUNIANI 1.KAMATI YA UCHANGUZI WANABURUZWA NA MWENYEKITI WA DMV AMEWAWEKA MKONONI HAKUNA WANACHOFANYA BILA YA KUPATA HUKSA YAKE. A) MWENYEKITI ANAYEGOMBEA KAWEKWA NA MWENYEKITI WA SASA WA DMV ILI MLINDIE MASLAHI YAKE ANAYOTAKA KUYAENDELEZA KUYAFANYA,HAWAKO HAPO KWA AJILI YA CHAMA WAKO KWA MASLAHI YAO WENYEWE 2.WAGOMBEA WALIYOJITOWA WAMEOMBA WAONGEZWE MUDA KWA SABABU KUBWA NA ZA MSINGI KWA MASLAHI YA CHAMA KUINGIZA WANACHAMA WAPYA ILI WAWEZE KUPIGA KURA HUYU MWENYEKITI WA SASA HAWEZI KUINGIZA WANACHAMA WENGI HAKUBALIKI NA HUYO ANATAKA KUMWEKA PIA HATA KUBALIKA KWA SABABU NI KIVULI CHA MWANYEKITI WA SASA DMV,MWENYEKITI WA SASA WA DMV ANAWAMBIA TUME YA UCHAGUZI WASIONGEZE MUDA KWA SABABU ANAJUWA VIZURI KWAMBA UKIONGEZWA MUDA MTU WAKE ANATAKA APATE UNYEKITI ATACHINDWA KAMA ALIVYOCHINDWA YEYE HAPO AWALI HAKI YA KUPIGA KURA ITATENDEKA WATAONDOLEWA 3.WAGOMBEA WAMEANDIKA BARUA ZA KUJIUZULU

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

Upuuzi mtupu!! kwa kweli ni wakati waangalie mambo ya msingi katika maisha yao na kujiuliza kwanini wako hapa kama tunaka kuingia ktk ulingo wa siasa tunafanya nini hapa walio wengi wako nyumbani nafikiri ukitaka kuleta mabaliko unabidi uwe katikati ya hiyo jamii kwa mawazo yangu nafikiri ingekuwa jinsi gani tutaweza kusaidia maendeleo ya nyumbani kuliko kuanzisha vyama ambavyo havitotupeleka popote kumbuka "fimbo ya mbali haiui nyoka" mabadiliko na mikakati huletwa na wale walio wengi nashauri nafasi hii iko nyumbani hapa ni ubabaishaji ambao mwisho wake hautakua mzuri kama unavyojionesha katika hatua za mwanzo.

Anonymous said...

NATAKA KUKUKANUSHA NA KUKUELIMISHA WEWE HAPO JUU ULIYEANDIKA KWA HERUFI KUBWA,,, SIDHANI KAMA UNAELIMU KWELI YA DARASANI AU UNA ILE YA CHINI YA MTI. HUYO MWENYEKITI ANAYETOKA AMEAMUA MWENYEWE KUTOKA NA ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMBEA NA WALA HAUSIKI KABISA NA KAMATI YA UCHAGUZI WEWE KWAKUWA UNA UFINYU WA AKILI UNASHINDWA HATA KUELEWA NINI KINAENDELEA UMEWAHI KUONA WAPI WANACHAMA WANAJIUNGA WIKI YA UCHAGUZI NA KWA TAARIFA YAKO UCHAGUZI HAUWEZI KUAHIRISHWA KWASABABU ZA KIPUUZI NA MWENYE MAAMUZI NI MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI NA SIO WA TAWI UNAONEKANA HUJUI LOLOTE..... NYIE NDIO WALE MNAOULIZA WANAFUNZI TANZANIA WAMEFELI SHULE ALAUMIWE RAIS... YEYE NDIO MWALIMU???? AU YEYE NDIO AFISA ELIMU AU WAZIRI WA ELIMU? KILA KAZI ZINA WENYEWE KAMA HUELEWI NYAMAZA SIO KUROPOKAROPOKA TUU...

Anonymous said...

Kwani tatizo liko wapi? Kama mnaona yote haya si muanzishe chama chenu tu cha washikaji vijana mpeane huo uenyekiti. Kelele nyingi za nini???

Anonymous said...

Hivi Kama unakipenda chama mbona mnalilia uongozi Hamna mshahara wala masilahi ni upenzi wa chama tuu yana anaelia hapa ni anaetaka uongozi na sio chama yani mmechemka sana Wewe unaelilia uongozi kwa manufaa yako jipange usingoje kutafuniwa kila kitu shame on you people mnatia aibu uongozi ni wito umefeli vibaya big up kamati