Kuanzia jumanne jioni tarehe 12/03/2013, idadi ya Makardinali 115 wa kanisa Katoliki kutoka sehemu mbalimbali duniani wameingia katika “conclave” ndani ya kanisa dogo maarufu kwa jina la Sistine tayari kwa shughuli hiyo nyeti kabisa ambayo itawachukua siku kadhaa. Awali ilitarajiwa Makardinali 117 kati ya 153 wenye sifa za kumchagua kiongozi huyo wa juu wa kanisa hilo wangefika makao makuu Vatikani kwa shughuli hiyo. Lakini kutokana na sababu za kiafya, Kardinali emeritus Julius Ruyadhi DARMAATMADJA ,sj kutoka Jarkata, Indonesia hakuweza kufika kwa sababu za kiafya, na Kardinali Keith O’Brien, ex- Cardinal toka Ediburgh, Scotland hakufika kwa sababu zake binafsi.
Hivyo watakaojisogeza katika “boksi” kumchagua kiongozi huyo ni 115 wenye umri chini ya miaka 80.B) Mgawanyo unaenda hivi:
Bara la Ulaya linawakilishwa na makardinali 60; wakitokea : Italia pekee ni : 28.
Ujerumani: 6.Uispania: 5. Polandi: 4. Ufaransa: 4. Austria: 1. Ubelgiji: 1.
Uswisi: 1. Ureno: 2. Uhaolanzi: 1. Ireland: 1. Jamuhuri ya Czech: 1.
Bosnia-Herzegovina: 1. Hungary: 1. Lithuania: 1. Kroatia:1. na Slovenia ni 1.
Bara la Amerika ya Kusini, maarufu pia kama Latino Amerika ni Makardinali 19; Wakitokea : Brazil: 5.
Mexico: 3. Argentina: 2. Kolombia:
1. Chile: 1. Venezuela: 1. Jamuhuri ya Dominikan : 1. Cuba: 1. Honduras: 1.
Peru: 1. Bolivia: 1. na Ecuador ni 1.
Bara la Amerika Kaskazini hasa Marekani ni Makardinali 14 ; wakitokea:
Marekani ni: 11. na Kanada: ni 3.
Bara la Afrika litawakilishwa na Makardinali 11:
wakitokea Nigeria: 2. Tanzania:
1. (Polycarp PENGO, Askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar-es-Salaam, Tanzania). Afrika ya Kusini : 1. Ghana: 1.
Sudan: 1. Kenya: 1. Senegal: 1. Misri: 1. Guinea: 1. Na Jamhuri ya kidemokrasia
ya Kongo ni : 1
Na bara la Asia litawakilishwa na makardinali 10: wakitokea India: 4. Ufilipino: 1. Vietnam: 1. Indonesia: 1. Lebanon:
1. China: 1. na Sri Lanka: 1.
Kati ya Makardinali 117wenye kupiga kura, 67 waliteuliwa na Papa Benedikti wa XVI. Wanaobakia 50 waliteuliwa na Papa John Paul II. --Kati ya hao walio hai ni 6 na ndiyo pekee walikuwepo wakati wa Mtaguso wa pili yaani tunaweza kuwaita (Council Fathers at the Second Vatican Council) nao ni Makardinali Angelini, Arinze, Canestri, Delly, Fernandes de Araújo, na Lourdusamy). Na waliosalia wana zaidi ya miaka 80 na hivyo hawataingia katika hiyo “Conclave”. -- Kati ya makardinali walio hai leo, 99 walishiriki katika uchaguzi wa mwaka 2005. Kati yao 49 tyari wana zaidi ya miaka 80 hivyo hawataweza kumchagua Papa mpya. (Baba mtakatifu Benedikti wa XVI naye alikuwa kati ya walioshiriki uchaguzi wa 2005.)
C) WANAOPIGIWA CHAPUO
Ikumbukwe kuwa viongozi hao walikutana Vatican ambako ni makao makuu ya Kanisa hilo na kuzungumzia maswala mbalimbali yanaloligusa kanisa na waumini wake. Kwa nyakati mbalimbali Makardinali hao walielezea maswala mbalimbali yanayoligusa Kanisa hilo kutoka katika maeneo yao.
Katika hali la “kuwachora” au kuwasanifu” jamaa kutoka kusini mwa jangwa la sahara, ambapo waandishi na watu mbalimbali wamekuwa wakiwadadisi kama kiongozi huyo atatokea bara hilo watajisikiaje. Sikatai kuwahoji mawazo na fikra pia maoni yao ni
vizuri. Lakini katika hali ya ukweli walikuwa wakiwa“chora” tu maana kwa sasa mtazamo na wakati wa kupata kiongozi toka ukanda huo unaonekana wazi kuwa bado wakati wake haujaiva. Pengine inawezekana maana ni kazi ya Roho Mtakatifu.
Wadadisi, watetesi wa mambo na vyanzo mbali mbali vinatabiria na kubashiri kuwa huenda majina haya yakatoka ndani ya “Conclave” hiyo kama Baba Mtakatifu, kiongozi wa kanisa hilo. Hii ni kwa mpangilio wa chagizo hizo.
1). K. ANGELO SCOLA, (71) Askofu
mkuu wa Jimbo kuu la Milan, Italia. 2). K. ODILO PEDRO SCHERER, (63) Askofu
mkuu wa jimbo kuu la Sao Paulo, Sao Paulo, Brazil.
3). K. MARC OUELLET, (68) kiongozi
mkuu mstaafu wa Maaskofu katika Roma, maarufu kama “Prefect Emeritus of the Congregation for Bishops” ni Askofu mkuu wa jimbo la Quebec, Canada-Francophonie.
4). LUIS ANTONIO
TAGLE, (55) Askofu mkuu wa jimbo la Manila, Ufilipino. Ndiye kijana wa pili kwa umri mdogo. Wadadisi wa mambo wanatabiri pia anaweza kuwepo kwenye uchaguzi ujao kama kandidate wa uongozi huo. 5).
K. FRANCISCO ROBLES ORTEGA, (64) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Guadalajara,
Jalisco, Mexico. 6). K. CHRISTOPH
SCHÖNBORN, (68) Askofu mkuu wa jimbo la kuu la Vienna, Austria. 7). K. JORGE MARIO BERGOGLIO, (76)
Askofu mkuu wa jimbo kuu la Buenos Aires, Argentina. 8). K. SEAN PATRICK O’MALLEY, (68) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Boston,
Massachusetts, USA. 9). K. PETER
ERDO, (60) Askofu mkuu wa jimbo kuu l’Esztergom-Budapest, Hungary. 10). K. ALBERT MALCOM RANJITH
PATABENDIGE DON, (64) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Colombo, Sri Lanka. 11). K. TIMOTHY MICHAEL DOLAN, (63) Askofu mkuu wa jimbo
kuu la New York, New York, USA. 12).
K. TELESPHORE PLACIDIUS TOPPO, (73) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Ranchi,
India. 13). K. JOAO BRAZ de AVIZ, (65) Askofu mkuu wa zamani wa jimbo kuu la
Brasilia, Brazil. Sasa anafanya kazi Vatican, Rome. 14). K. FERNANDO FILONI, (66), Italia, Kiongozi wa ofisi ya uinjilishaji makao makuu Vatican. 15). K. Leonardo SANDRI, (69) Argentina, Anafanya kazi makao makuu Vatican.
D). WAKATI KANISA LIKIKUWA
ZAIDI NCHA YA KUSINI, UONGOZI UNABAKI KWA KIASI KIKUBWA HAPA ULAYA.
Zaidi ya karne moja iliyopita
ukuaji wa kanisa, idadi ya waumini inaongezeka nje ya bara Ulaya na sasa kuna wastani
wa zaidi ya waumini milioni 200 wa kanisa Katoliki wapo katika bara la Latini-Amerika ukilinganisha na Ulaya. Ukiangalia kwa makini Makardinali toka bara la Ulaya wanakaribia nusu ya wapiga kura wote. Ikumbukwe kuwa ili kumpata baba mtakatifu, inatakiwa achaguliwe na zaidi ya kura 77 ; kati ya 115.
Mlinganisho wa kimabara wa idadi ya waumini wa kanisa hilo katika mamilioni ni makadirio ya karibu.
Latin Amerika -----Milioni 484;
Ulaya----------Milioni 278;
Afrika -----Milioni 178; Asia------- Milioni 138;
Amerika ya Kaskazini ----Milioni 86; Osheania (Oceania) -------Milioni 10.
Kisio la mgawanyo wa waumini wa Kanisa Katoliki
ki-nchi katika kisio kwa mamilioni. Awali ya yote ikumbukwe kuwa Brazil ndiyo
nchi yenye wakatoliki wengi duniani. Uchunguzi unaonyesha Brazil ikiwa na
wastani wa Millioni 150 ya wananchi wake ni waumini wa kanisa hilo.
Idadi hii ni katika mamilioni.
Brazil 150; Mexico 100; Ufilipino 76; Marekani 74; Italia 57; Ufaransa 45;
Colombia 42; Uhispania 42; Poland 36; Argentina 36; Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo 36; Ujerumani 28 ; Peru
27 ; Venezuela 26 ; Nigeria
22 ; India 19 ; Canada 15 ;
China 16 ; Tanzania 15 ; Uganda 15 ; Equatorial(Equador)
13 ; Chile 12 ; Angola 11 ; Ureno 11 ; Uingereza 10 ; Kenya 9.
Tunaona bara la Amerika ya
Kusini ndilo bara lenye wakatoliki wengi kuliko mabara mengine. Afrika inaonyesha kuendelea kukua kwa kasi kwa kuwa na idadi ya waumini wa kanisahilo. Bara Asia linaonyesha kuendelea kuongeza idadi ya waumini wakanisa hilo kwa siku za usoni. Kwa Afrika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiyo
inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya Wakatoliki ikifuatiwa na Nigeria ya tatu ikiwa ni TANZANIA ikifuatiwa na Uganda kwakaribu kabisa. Halafu Angola inafuatia huku Kenya ikifuatia.
Imeandaliwa
na Frédéric Meela, Paris
kwa msaada wa vyanzo mbalimbali.
Chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment