Suala kubwa ni kwamba, hakuna raha katika kuchangia penzi na wengi wanaamini penzi haliwezi kugawanyika hivyo mwanaume anapoamua kuwa na wake wawili ama zaidi, ajue lazima kati ya hao mmoja atajisikia mnyonge, asiyependwa.
Kwa kuonesha wanawake wengi wanachukia uke wenza, pale mwanaume anapomtajia mkewe suala la kuongeza mke wa pili ni lazima utasikia; “Ukileta mke mwingine, mimi naondoka, kwani unakosa nini kutoka kwangu, kama kuna kitu ambacho hukipati si useme tu?”
Kwa sababu hiyo ndiyo maana kasi ya kuoa wake zaidi ya mmoja hivi sasa imepungua.
Hata hivyo, kufuatia wanawake wengi kuchukia uke wenza, baadhi ya wanaume wamebuni njia nyingine ya kutimiza azma yao kwa kuwa na nyumba ndogo.
Wapo ambao tunapozungumzia nyumba ndogo hawaelewi tunazungumzia kitu gani. Kwa tafsiri ambayo siyo rasmi kutokana na neno lenyewe kutokuwa rasmi katika Kiswahili, ni mwanamke ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye tayari ameshaoa, ama ana mpenzi wake.
Wanaume wengi hujitahidi sana uhusiano huo kuwa wa siri huku wakijua kwamba ukifahamika unaweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa kama siyo kuleta mvurugiko ndani ya nyumba.
Licha ya kuwepo kwa usiri katika hilo, bado wanawake wengi huwa wanahisi hakuna mwanaume asiye na nyumba ndogo huku wakisisitiza kuwa, bora wasijue yupo mtu ambaye wanachangia naye penzi kuliko kujua.
“Hakuna kitu ambacho kinaniuma kama kusikia mume wangu ana uhusiano na mwanamke mwingine, bora nisijue japo kuna uwezekano ana uhusianao na mwanamke mwingine. Wanaume kwani wanaridhika?” anaeleza mama mmoja anayeonesha kuamini wanaume wengi wana nyumba ndogo.
Ukitaka kuthibitisha kwamba wanawake wengi wanahisi waume zao kuwa na nyumba ndogo, kuna siku unapompigia simu mke wako si ajabu akakuuliza “Eeh Dear! Uko wapi? Uko na nani au uko na nyumba ndogo?” anaongea hivyo kwa utani tu lakini ukweli ni kwamba wanawake wengi wanapokuwa mbali na waume zao hufikiria ni lazima watasalitiwa hata kama hakuna ukweli wowote juu ya hilo. Ni kushindwa tu kujiamini.
Sikatai wapo baadhi ya wanaume ambao wana ‘vijumba vidogo’ vingi tu.
Wanaume wanaofanya hivyo ndiyo wanaoipa nguvu ile sheria ya dini ya Kiislam ya kusema mwanaume unaruhusiwa kuoa wake zaidi ya mmoja.
Kama unaona mke mmoja hakutoshi kwa nini usiamue kuoa tu mke mwingine kuliko kuwa na kimada?
Itaendelea wiki ijayo.
Global Publishers
2 comments:
bora uke wenza kane mkitafakari hili mwanamke anapewa haki yake katika uke wenza kuliko kuwa kimada wa pembeni na mtoto/watoto wakizaliwa wanakosa haki angaliye jinsi mambo yanavyo dhihirika hata wazungu siku hizi wanakubali uke wenza cheki picha hapo juu ukadi wenu tuu tiyeni timu ndani mke apate stara watu wapunguze kuwa vichecheee
Wanaume wenye tamaa hata awe na wake wanne, bado atataka wa tano, 6,na bado ata cheat tu! Tatizo ni tamaa ya mwili iliyozidi ya kawaida! Wazungu wanaita sex addiction! Na hakuna mapenzi ya kugawanywa kama karanga, na eti
kila mtu apate sawa, humuoni wala kumsikia huyo mume anavyokuwa anafanya au kuongea na mke mwenzio! Utasemaje mnapewa penzi sawa? Ni mila, utamaduni, dini, na uamuzi wa watu mbalimbali! Hivyo tutabaki kuheshimu watu na maamuzi yao ktk mapenzi.
Post a Comment