ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 21, 2013

Wahabeshi 47 wafungwa miezi sita jela

Tanga. Hatimaye, wahamiaji haramu 47 wa Ethiopia waliokamatwa wakiwa wanasafirishwa ndani ya makontena, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kuishi nchini isivyo halali.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde,baada ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani kwamara ya pili, kufuatia kupatikana kwa mkalimani wa lugha ya kwao.

Kabla ya hukumu hiyo, Mwanasheria wa Idara ya Uhamiaji mkoani Tanga, Adam Kinyamagoha, alidai kuwa washtakiwa walikamatwa Machi Mosi mwaka huu katika Kijiji cha Kitumbi, wilayani Handeni. Alidai kwamba watu hao walikamatwa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani baada ya kuyasimamisha malori aina ya Scania yanamilikiwa na Kampuni ya Charan Sigh $ Sons Ltd na kusikia kelele za kugongwa kwa makontena yaliyokuwa yakisafirishwa na malori hayo.

Alisema ‘baadaye ofisa huyo wa polisi aliamuru yafunguliwe.”
Hakimu Maira aliwataka ama kulipa faini ya Sh50,000 kila mmoja au kwenda jela miezi sita.
Mwananchi

No comments: