Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansoor Yussuf Himid, alipowasili katika viwanja vya Pwani ya Mazizini kuzindua Soko la Samaki.
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe kushoto akimuonesha picha za maeneo yaliotoswa matumbae ya kutengeneza, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya kutembelea Maendeleo ya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Wavuvi wa Dago la Mazizini Pwani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia baada ya kuwafungulia Soko lao la Samaki, lililojengwa kwa nguvu za Wananchi na Mradi wa Tasaf Unguja.
Boti za Patro za Idara ya Uvuvi Zanzibar ambazo hutumika katika kufanyia doria katika bahari ya Zanzibar kupambana na Wavuvi haramu wanaoharibu mazingira ya baharini.
Mkurugenzi Mkuun wa Viwanja vya Ndege Zanzibar Said Tumbugani akimuonesha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein, michoro ya ramani ya maeneo ya Barabara ya kuondokea ndege na maegesho ya ndege yanayojengwa katika kiwango cha kimataifa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar wakati wa ziara yake.
kwa picha zaidi bofya read more
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Dk. Malik Akili , alipokuwa akitembelea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.kulia Waziri wa Mawasiliani Rashid Seif Suleiman.
Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Zanzibar Said Tumbugani akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar alipotembelea uwanja huo.
Ofisa wa Kampuni ya Sogea Satom inayojenga Barabara ya kuondokea ndege na maegesho ya ndege Roberto Sapone akimuonesha maeneo ya ujenzi huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipofanya ziara kutembelea ujenzi huo kuona maendeleo yake, wakati waziara yake Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Zanzibar Dk. Akil akimoonesha Rais wa Zanzibar Jengo la Abiria wakati wa ziara yake.
Picha kwa hisani ya Zanzi News
No comments:
Post a Comment