ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 5, 2013

COMORO YAHIMIZA UHUSIANO ZAIDI NA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mhe.Lily Munanka (kulia) akisalimiana na Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro Ubalozini Tanzania House Washington DC.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro katika picha ya pamoja na Mhe.Lily Munanka, Kaimu Balozi.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro akisalimiana na Suleiman Saleh,(kulia) Afisa Ubalozi wa Tanzania,Washington DC.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro (katikati) katika picha ya pamoja na Suleiman Saleh,(kulia) Afisa Ubalozi wa Tanzania,Washington DC. Kushoto ni Mhe.Lily Munanka Kaimu Balozi.

Balozi wa visiwa vya Comoro nchini Marekani Mhe. Roubani Kaambi jana alitembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania (Tanzania House) Washington DC na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka ambayo yalilenga katika kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Balozi Roubani ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Visiwa vya Comoro katika Umoja wa Mataifa alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Comoro kuimarisha zaidi mahusiano yao kihistoria na kuyatafsiri mahusiano hayo katika mashirikiano zaidi kiuchumi. Balozi Roubani alibainisha kwamba nchi yake inafahamu mafanikio mbali mbali katika sekta za uwekezaji pamoja na utalii na hivyo kuomba nchi yake isaidiwe kuwavutia wawekezaji kutoka Marekani pamoja na kukuza utalii kutokana na mazingira ya nchi yake kufanana na yale ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa upande wake Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka alimshukuru Balozi Kaambi kwa kumtembelea na kumweleza kwamba kimsingi ameyapokea maombi yake hayo na atayawasilisha katika mamlaka husika ili yatolewe maamuzi stahili. Kwa ujumla Kaimu Balozi Munanka alimhakikishia Balozi Kaambi kwamba Tanzania inathamini mahusiano baina ya nchi zao na kuona umuhimu wa kujenga mashirikiano zaidi kiuchumi baina ya nchi zao mbili kwa faida ya wananchi wao,

No comments: