Dar es Salaam.Makamu Mwenyekiti wa Simba aliyejiuzulu, Geofrey Nyange Kaburu amewashangaa watu wanaomhusisha na vitendo vya kuihujumu timu hiyo katika michezo yake ya Ligi Kuu inayoendelea.
Akizungumza na Mwananchi, Kaburu alisema watu wanaomshutumu kuihujumu timu wana nia ya kumchafua na kumgombanisha na Wanasimba wenzake bila ya sababu za msingi.
Alisema wachezaji wote waliosajiliwa na Simba ni mali ya klabu ya Simba na wanalipwa mishahara na klabu ya Simba na siyo mtu binafsi.
Alisema wachezaji wote waliosajiliwa na Simba ni mali ya klabu ya Simba na wanalipwa mishahara na klabu ya Simba na siyo mtu binafsi.
‘’Watu wanashindwa kujiuliza baada ya kuchukua ubingwa msimu uliopita Simba imewapoteza nyota wake Kelvin Yondani, marehemu Patrick Mafisango na Emmanuel Okwi, Nafasi zao zimezibwa? Wanatakiwa kujiuliza hivyo na siyo kuchafua watu.’’
“Tatizo la Simba lilikuwa katika safu ya ulinzi, lakini halikuzibwa, wamemuuza Okwi pia nafasi yake haikuzibwa sasa leo watu watasema wachezaji wanatumika kuhujumu timu hiyo, siyo kweli, sababu ni mapengo ya baadhi ya wachezaji hayakuzibwa,” alisema Kaburu.
Alisema yeye bado ni mwanachama halali wa Simba na ataendelea kutoa michango yake kama mwanachama na endapo atachaguliwa katika kamati yoyote yupo tayari lakini baada ya kumaliza matatizo yaliyopo katika klabu hiyo kwa sasa.
Katika hatua nyingine, Kaburu amesema hakuhitaji kujadiliwa na Kamati ya Utendaji ya Simba kwa kitendo chake cha kujiuzulu kwa kuwa alitimiza wajibu wake wa kuwajibika baada ya kuona mambo hayaendi vizuri katika klabu yake.
Hivi karibuni Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe walitangaza kujiuzulu nyadhifa zao katika klabu hiyo baada ya kuona timu haifanyi vizuri.
Hata hivyo, juzi Kamati ya Utendaji ya Simba ilitangaza kumrudisha Hans Poppe kundini huku wakiridhia kujiuzulu kwa Kaburu.
Hata hivyo, juzi Kamati ya Utendaji ya Simba ilitangaza kumrudisha Hans Poppe kundini huku wakiridhia kujiuzulu kwa Kaburu.
Kaburu alisema kuwa alichokifanya ni sahihi na hata katiba ya Simba inaruhusu kufanya hivyo, hakukuwa na suala la kumjadili kwani hata kama angetakiwa kurudi Simba kwa sasa asingekubali kwa kuwa yaliyomfanya ajiuzulu bado yapo.Text inakuja hapa.
Mwananchi
1 comment:
Bw.Kaburu wadanganye waliokuwa hawaujui mpira wa Simba na Yanga. Huko nyumba Simba ilihujumiwa na Kassim Dewji na kundi la Friends of Simba wakati Phiri akiwa kocha. Phiri alionywa asiwapange Kaseja,Pawasa,Matola na akaambiwa kwamba watahujumu mechi ya Simba na Moro United Morogoro.Phiri alipuuza na dakika 20 Simba 0 Moro 3.Akafanya mabadiliko ya wachezaji tajwa Simba ikarudisha goli2 na kufungwa 3-2. Kwa hiyo huo ni mchezo mchafu na Kaburu ana mkono tu kwani kuna wachezaji wamesajiliwa na yeye na wanaomtuma.
Post a Comment