Kadogo alipokuwa Hospitali akiuguza majeraha, kabla ya kukatwa miguu, aliyesimama ni mama yake mzazi ambaye sasa ni marehemu
Ni miaka 12 sasa ya maisha magumu kwa Kadogo Waya Daudi (33) tangu akatwe miguu yote baada ya kupigwa na kisha kumwagiwa maji ya betri na mume wake kutokana na wivu wa kimapenzi.
Akiwa bado msichana mdogo wa miaka 18 na ndoa yake ikiwa imedumu kwa miaka miwili tu, Kadogo hakujua kama ndoa hiyo ingegeuka kuwa shubiri katika maisha yake.
Ilivyotokea
Kabla ya kutoa simulizi yake iliyojaa simanzi, anatoa sharti la kuitwa Kadogo Marwa Bwiyagi jina la baba yake mzazi kwa madai kuwa anaposikia jina la Daudi ambaye alimfanyia unyama huo, hujisikia vibaya na kukubaliana na sharti hilo.

Huku akizungumza kwa vituo anasema Agosti 4, 2000 ni siku ambayo hataisahau maishani, kwani historia ya maisha yake ilibadilika kutoka msichana mrembo na kuwa msichana mlemavu asiyekuwa na miguu.
Akiwa anaishi katika kitongoji cha Zahanati kijiji cha Rung’abure wilayani Serengeti na mume wake, wakiwa na mtoto mmoja wa kike Neema (2), Kadogo alikwenda kuuza ndizi mbivu mjini Mugumu zenye thamani ya Sh5,000 ili apate fedha za kuhudumia familia.
“Mume wangu pamoja na kuwa alikuwa haachi pesa ya mboga, lakini akikuta mboga asiyoipenda hakukaliki…, nikawa nikitoka shamba napeleka ndizi mjini, nikiuza nanunua mboga na mahitaji mengine… lakini akawa ameweka muda wa mwisho kuingia nyumbani ni saa 12:00 jioni.
“Kwa kuwa siku hiyo ndizi zilichelewa kwisha, nilichelewa kidogo kurudi nyumbani, ilinibidi nikimbie masafa ya kilometa 25 huku nikiwa nimebeba kilo moja ya nyama, nikafika nyumbani saa 12:30. Bila hata kuniuliza, akatoa hukumu kuwa kuchelewa kwangu nilikuwa na mwanamume…,” anasimulia Kadogo.
Licha ya Kadogo kujaribu kujitetea kwa kumweleza kuwa alichelewa kumaliza biashara, lakini hakukubali, zaidi ya kwenda kukata mzigo wa fimbo,
kwa madai kuwa uzuri wake unamzuzua, wanaume wanamfuatafuata. Kadogo alikimbilia kwa wifi yake ili kuomba msaada, hata hivyo haikusaidia, kwani hakuweza kukwepa adhabu ya kikatili. Alivuliwa nguo na kufungwa darini.
“Daudi bila chembe ya huruma alinifanyia unyama wa kutisha…, alinivua nguo zote, akanifunga kwa kamba miguu na mikono kisha akanifunga darini…, akaanza kunichapa nikiwa nimening’inia, alinichapa sana huku akitishia nikipiga kelele ndiyo mwisho wangu…nilitii,” anasimulia Kadogo huku akijifuta machozi.
Mahojiano haya yanahitaji uvumilivu kutokana na hali ya Kadogo akumbukapo madhila aliyopata humwaga chozi, alisema mwili ulijaa damu, lakini hakumhurumia, aliokolewa na mpita njia baada ya kusikia kinachoendelea, ambaye alitoa maneno yaliyomchoma Daudi na hapo ndipo alipositisha adhabu. “Alimwambia ….piga uue…kesho tuje kwako kuchimba kaburi, kauli hiyo ilimstua, ghafla akaacha kunipiga.
Aliponifungua kamba, mwili wangu wote ukawa umekufa ganzi. Alipoona hali yangu imekuwa mbaya alikimbia kwa dada yake, akamwambia aje anikande. Haikusaidia, maana hali ilikuwa mbaya
Amwagiwa maji ya betri
Akiwa anauguza vidonda huku amefungiwa ndani kwa siku nane bila matibabu yoyote , mume wake alifika na maji ya betri ambayo alimwambia kuwa ni tindikali, inasaidia kuponya vidonda na kumwagia kwenye vidonda miguu yote .

“Maumivu yalikuwa makali sana…, kwa kweli niliteseka sana, yeye hakujali, baada ya muda mwili ukabadilika, nyama zikaanza koza na kudondoka, huku najiangalia. Akawa ananifungia ndani, akitoka anafunga kufuli kwa nje, majirani wakadhani nimesafiri.
Hata hivyo baada ya kufuatilia walibaini nimo ndani, wakatoa taarifa ofisini, akaamriwa kunipeleka hospitali…, alipoambiwa tunapitia PF3 polisi, akatoroka sijamwona tena,” anasema Kadogo.
Hata hivyo pamoja na juhudi za waganga, wauguzi na madaktari wa hospitali teule ya Nyerere DHH kumtibu, hali ilizidi kuwa mbaya maana miguu ilikuwa inaoza na ndipo walipoamua kumkata miguu yote.
Mwaka 2001 akatwa miguu
Mwaka 2001 ili kuokoa maisha yake, madaktari walisema kuwa sumu hiyo inazidi kunyofoa nyama hivyo miguu ikatwe kwa kuwa ilikuwa imeharibika na kumlazimu kukaa hospitali kwa miaka mitatu.
Mwaka 2001 ili kuokoa maisha yake, madaktari walisema kuwa sumu hiyo inazidi kunyofoa nyama hivyo miguu ikatwe kwa kuwa ilikuwa imeharibika na kumlazimu kukaa hospitali kwa miaka mitatu.
“Kipindi chote hicho marehemu mama yangu Elizabeth Gibayi, ndiye aliyekuwa akihangaika nami, nilikuwa siwezi kusimama wala kukaa ni kulala tu. Nikumbukapo mateso hayo natamani ningetangulia mimi nikamwacha mama yangu,” anamwaga chozi.
Maisha baada ya kutoka hospitali
Kadogo anasema kuwa maisha yake ni magumu, kwa kuwa aliowategemea wote sasa ni marehemu ambao ni mama na kaka yake.
Kadogo anasema kuwa maisha yake ni magumu, kwa kuwa aliowategemea wote sasa ni marehemu ambao ni mama na kaka yake.
“Mama yangu alifariki mwaka 2005. Mwaka 2011 kaka ambaye naye alikuwa nguzo akaaga dunia, ndugu wengine hawajali nimebaki mpweke,” anasema kwa huzuni.
Apata mpenzi mpya
Mapenzi ni hisia humpata kila mtu, ndivyo ilivyokuwa kwa Kadogo baada ya kupona, alimpata mpenzi mpya Samson Pius (32) akiamini yeye nitofauti na mume wake aliyemfanyia ukatili, tena kwa hali aliyokuwa nayo akamwona ana upendo wa kweli, kukubali mwanamke asiye na miguu.

“Tuliishi naye miaka tisa, tukazaa watoto wanne, Frank Isaya (9) darasa la tatu, Juma Gibayi (7) darasa la pili, Ayubu Gibayi (4) darasa la awali, wote wanasoma Shule ya Msingi Mapinduzi “A” na wa mwisho ni Anna Gibayi (2) ambaye bado ananyonya. Bwana huyu aliyenizalisha watoto wanne naye amenikimbia kwa madai kuwa mzigo umekuwa mkubwa, nami sizalishi, kaniachia watoto nahangaika nao,” anasimulia kwa huzuni.
Afungwa kwa kuuza gongo
Kutokana na majukumu ya kumzonga, anasema alilazimika kuuza pombe haramu ya gongo katika mtaa anaoishi wa Starehe Mbege, ili aweze kuhudumia familia yake, kulipa kodi, kununua chakula na mahitaji mengine, lakini alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja.

“Kwa sasa nauza ndizi, mkaa, nyanya na sabuni ili niendeshe maisha, lakini hali ni ngumu maana kutembea kwangu natumia magoti, nilipewa baiskeli lakini imeharibika na utengenezaji unakuwa mgumu kwa kukosa fedha,” anasema Kadogo.
Mtoto ameshindwa kujiunga na sekondari kwa kukosa karo.
Anasema yeye aliishia darasa la kwanza kutokana na mazingira ya nyumbani kwao na kulazimika kuolewa mapema, lakini mwanawe amefaulu kujiunga na kidato cha kwanza Serengeti sekondari, lakini uwezo wa kumsomesha hana.
“Pamoja na kuwa ni shule za kata lakini mahitaji yanagharimu karibu Sh350,000.
Michango mingi wameorodhesha …, mimi sina pesa, nimemwambia akae tu siku akipatikana msamaria mwema wa kumsomesha, amsaidie.
Hali yangu kila mmoja anaiona, kula kwangu ni mbinde…. Nilikuwa na nguvu za kulima, kufanya biashara, lakini sasa siwezi tena,” anasema Kadogo huku akitokwa machozi.
Neema Nyangige
Neema (14) anasema akipata msaada ataanza masomo wakati wowote,” nadhani elimu pekee ndiyo inayoweza kuwa msaada kwangu, wadogo zangu na mama yangu.
Neema (14) anasema akipata msaada ataanza masomo wakati wowote,” nadhani elimu pekee ndiyo inayoweza kuwa msaada kwangu, wadogo zangu na mama yangu.
Nikipata msaada naenda shule, ikiwezekana nikae huko ili nisome vizuri kwa sababu kwa mazingira ya nyumbani sitaweza kujisomea, ni magumu sana,” anasema kwa uchungu.
Barua ya maagizo ya kujiunga na sekondari yenye kumb. Na SS/JI/VOL.12013 ya Desemba 21, 2012, imeorodhesha vitu na michango mingi ambayo imekuwa kikwazo kwa mtoto huyo.
Licha ya kuwapo mpango wa kusomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupitia Kamati ya Ukimwi, kutokana na fedha wanazopata toka Tacaids, familia hiyo licha ya kutembelewa na viongozi kutoka katika ofisi za kitongoji na wilaya, bado Neema hajasaidiwa ili aanze masomo.
Ogada Magati kaimu Ofisa Mipango anasema tatizo hilo wanalifahamu na kwamba anategemea kuwasilisha kwenye kikao cha wataalamu ili asaidiwe kupitia Tacaids.
”Tumetembelewa na wageni toka Tacaids makao makuu, tunajua tatizo lake nategemea kufuatilia shuleni ili aruhusiwe kuanza masomo wakati tukiendelea na mchakato wa kumsaidia,” anasema.
Hata hivyo ni mwezi karibu wa tano sasa, hakuna kilichokwishafanywa na halmashauri, ofisi ya mbunge wala mkuu wa wilaya licha ya kutumia DVD za mama huyo kwenye makongamano kama ushuhuda wa madhara ya ukatili.
Wanawake wazungumzia ukatili
Monica Daniel ni katibu wa shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu Serengeti (Washehabise), anasema vitendo vya ukatili kama hivyo vinatokana na mfumo dume ambao umekita mizizi hasa katika Mkoa wa Mara ambako mwanamke anamilikiwa kama bidhaa kutokana na wanaume kutoa mahari ya kiasi kikubwa.

“Kwenye Katiba Mpya tunataka mambo haya yawekwe bayana…, haki za mwanamke ziainishwe na ziwekewe vyombo na sheria za kuzilinda.
Kwa atakayeguswa na matatizo ya Kadogo, apige simu namba 0759 891849, 0713 290944 au 0787 239480.
Kwa atakayeguswa na matatizo ya Kadogo, apige simu namba 0759 891849, 0713 290944 au 0787 239480.
Mwananchi
3 comments:
KIlio cha wanawake sijakisiakia bado kutokana na ukatili huo aliofanyiwa mwanamke mwenzetu. Kama huyu dada angekuwa anaitwa Wema Sepetu, nafikiri tungeandamana dunia nzima bila kuvaa nguo.
Yani hii story imeniliza, but nimejikuta nanyamaza ghafla nipo anza kusoma hii paragraph.........."
Ogada Magati kaimu Ofisa Mipango anasema tatizo hilo wanalifahamu na kwamba anategemea kuwasilisha kwenye kikao cha wataalamu ili asaidiwe kupitia Tacaids.
”Tumetembelewa na wageni toka Tacaids makao makuu, tunajua tatizo lake nategemea kufuatilia shuleni ili aruhusiwe kuanza masomo wakati tukiendelea na mchakato wa kumsaidia,” anasema.
Hata hivyo ni mwezi karibu wa tano sasa, hakuna kilichokwishafanywa na halmashauri, ofisi ya mbunge wala mkuu wa wilaya licha ya kutumia DVD za mama huyo kwenye makongamano kama ushuhuda wa madhara ya ukatili.
Wanawake wazungumzia ukatili
Monica Daniel ni katibu wa shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu Serengeti (Washehabise), anasema vitendo vya ukatili kama hivyo vinatokana na mfumo dume ambao umekita mizizi hasa katika Mkoa wa Mara ambako mwanamke anamilikiwa kama bidhaa kutokana na wanaume kutoa mahari ya kiasi kikubwa."
Hivi kwanini jamani wabongo wako hivi, yani hawana huruma kabisa, matatizo ya watu wao wanageuza mitaji, na sehemu za kutafuta ucelebrity usio na mpango? Dj-Luke please promote hii issue, ile watu wajue kuwa this is how TACAIDS nivyo hujumu pesa za misaada, hawa watu napewa pesa nyingi sana, lakini zinaishia mifukoni mwao, it's about time to ashame them!! Please, sambaza hizi kwa blog nyingine au fungulia facebook A/C ili watu wachangie.
Jamani, this is not a story haya ni maisha ya mtu. Kwanini huweki simu au adress ili watu waweze kumsaidia?
Post a Comment