ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 3, 2013

KILICHOSEMWA NA SHIRIKA LA NYUMBA KUHUSU KIWANJA CHA GOROFA LILILOANGUKA DAR


Shirika la nyumba la Taifa NHC limekiri kwamba ndio mmiliki wa kiwanja kilichokua kimejengwa jengo la gorofa 16 ambalo liliporomoka siku kadhaa zilizopita Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu 36 na kujeruhi 18.

Mkurugenzi Mkuu Nehemia Mchechu amesema kwa kawaida shirika la nyumba limekua likiingia ubia na watu binafsi wenye uwezo wa kujenga nyumba kama hizo ambapo liliingia ubia na kampuni ya ujenzi ya RAZA na kusaini mkataba wa kujenga jengo lenye gorofa 10 tu kwenye eneo hilo ingawa baadae kampuni hiyo iliomba kubadili mkataba ili wajenge gorofa 16.
Kuhusu umiliki kwa asilimia 25 kwenye jengo lililoporomoka, Mchechu amesema kwa ubia uliokuwepo walipaswa kupewa asilimia hizo baada ya ujenzi kukamilika na asilimia nyingine 25 wangepewa miaka kumi baadae kulingana na mkataba na hawakupaswa kuhusika kwenye gharama zozote wala taratibu za ujenzi.

Namkariri akisema “february 15 2011 ndio walituandikia kwamba wanakusudia kuongeza ghorofa zifike 16 na kwamba wanawasiliana na Mamlaka husika kwa ajili ya kupata vibali hivyo na wakifanikiwa wangeomba kuongezewa muda wa kumaliza mradi na pia baada ya kupata kibali wangetutaarifu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya mkataba”

Kwenye line nyingine, NHC imeunda timu kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika miradi yake yote ya ujenzi wa ubia ili kujihakikishia usalama wa majengo husika.

www.Millardayo.com

2 comments:

Anonymous said...

siajabu hata baadhi ya wakubwa wakawa responsible kwa hiyo issue kwan haiwezekan jengo lina jengwa chin ya kiwango haraf mainjinia na macontractor wanaona haraf wakawe kimya nashauri mheshimiwa prof anna tibaijuka asimamie mwenyewe kwa kuunda tume atakayo jilidhisha nayo kufanya uchunguz,
aidha shirika la nyumba la taifa nivema likaingia mikataba na makampuni yenye vigezo kuliko kuua watu tegemez na wasio na hatia yoyote
its me ezra wa ruco sheria

Anonymous said...

Kila ghorofa inabidi liundiwe tume za watu atleast 24. Na hizo tume zikichelewa kutoa majibu inabidi nazo ziundiwe tume za kuzichunguza. Tume za uchunguzi nazo zikichelewa basi iundwe tume ya kuchunguza tume za uchunguzi. Hapo tutakuwa salama.