ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 2, 2013

MAPENZI NI KUHAMA ULIMWENGU WA KAWAIDA NA KUZAMA KWENYE ‘MALAVIDAVI’ -3


MDAU wa kona hii, leo tunamalizia mada hii iliyoanza wiki tatu zilizopita. Tuwe pamoja kwani naamini utapa darasa litakalo kusaidia katika maisha yako ya kimapenzi na umpendaye...

Onesha mabadiliko, muoneshe jinsi unavyoridhishwa na upendo wake kisha mtamkie kwamba kwake umefika, halafu thibitisha hilo kwa vitendo.

MVUTO (Attractiveness)
Wanaume huhitaji wapenzi wao wawe na mvuto. Hii inawezekana isiwe na maana kwa wanawake kwa kushindwa kutambua jinsi mvuto wao unavyoweza kuwa kibwagizo murua cha mapenzi.
Vaa vizuri upendeze, hakikisha muda wote unakuwa nadhifu. Muonekano wako ndiyo utamfanya mwenzi wako ajiamini popote. Kwa hiyo, kupendeza kwako ni bonge la chombezo kwa mwenzio.

UAMINIFU (Trustful)
Wanaume hupenda wanawake wenye uaminifu wa asilimia 100. Mwanaume huhitaji mwanamke ambaye muda wote atakuwepo kwa ajili yake kimapenzi, kubadilishana mawazo na kumshirikisha katika siri za maisha yake.
Bahati mbaya wapo wanawake wengi ambao hawana uaminifu hata chembe. Hilo huwafanya wanaume kukosa imani kwa wapenzi wao. Jiamini kisha uwe muaminifu. Mfanye mpenzi wako asikutilie shaka ya aina yoyote kisha uone jinsi maisha yanavyoweza kusonga mbele.

FAMILIA (Family)
Wazo la kila mwanaume anapopata mwanamke, hufikiria ajenge naye familia haraka iwezekanavyo. Hivyo basi, huhitaji mwanamke ambaye yupo tayari kwa hilo. Kitu ambacho huwakera wengi ni pale wanapokutana na mtu aliye na mawazo ya kurukaruka.
Kama umeshaolewa, muoneshe mumeo jinsi ulivyo fundi wa kuiweka familia pamoja. Ukifanya hivyo, utakuwa umempatia, kwani hakuna jambo ambalo wanaume huwa hawapendi kama kuona familia inasambaratika.

UKARIMU (Kindness)
Wanaume huwa na matarajio ya kuwaona wanawake wao wakiwa wapole, waungwana na wakarimu. Jitazame na ujitengeneze kuwa hivyo ili umvutie mwenzi wako. Ukorofi, ubishi na roho mbaya siyo sifa ya kike.

UCHESHI (Funny)
Wanaume hupenda wanawake wanaojua kucheka. Akiwa naye, wazungumze na wacheke. Wanaume huwachukia wanawake wanaopenda kununa. Kama una tabia hiyo, jirekebishe ili umkune mwenzi wako.

UANAMKE (Femaleness)
Kwa kawaida, wanaume hupenda wanawake ambao wanajitambua kuwa wao ni wanawake. Huwachukia wale wanaojipa sifa ya u-dume au wababe, wanaopenda kutoa amri.
Huhitaji wanawake wanaotimiza wajibu wao kama wanawake kulingana na jamii inavyotambua. Hupenda wanawake wanaojali, kujiheshimu na kadhalika. Wale walevi hukosa sifa ya Uanamke ambayo wanaume huihitaji.

Global Publishers

No comments: