Mshindi na ambae atakuwa bingwa mpya wa Universal Boxing Organization uzito wa light fly kati ya Issa omar(peche boy) na Shaban Madilu amepata shavu la kucheza may 18 na lienel legada ambae ni bondia bingwa wa ufilipino.Pambano litakalo fanyaka katika mji wa Dumaguete City, Negros Oriental nchini philipines . Ofa hiyo imekuja baada ya vyama vya ngumi kupitia record zao na kuwashauri mabondia hao kucheza ubingwa wa UBO(Universal Boxing Organization) ambao nao pia upo wazi kutokana na bingwa aliepita kutoutetea kwa kipindi kirefu. UBO kupitia mwakilishi wao kanda ya Africa mashariki ndg Emmanuel Mlundwa imekubali pia kudhamini pambano hilo kwa kutoa ubingwa huo kwa mabondia wawili toka nchi moja yaani Tanzania kugombania ubingwa huo. Nafasi ambazo ni chache sana kutokea bahati kama hiyo, pindi itakuwa na muda mfupi wa kuutete ubingwa huo kwa ofa hiyo ya ufilipino ambayo itakuwa na ukishirikishwa wa ubingwa wa PAN PACIFIC lightfly weight title nchini ufilipino mwishoni mwa mwezi ujao kulingana hali ya bondia na matokeo ya mpambano wa tarehe 7 april utakao fanyika katika ukumbi wa ccm mwinjuma-mwananyamala. Ni mpambano ambao pia utawakutanisha mabondia wengi wakongwe na chipukizi
IBRAHIM KAMWE
Director - Bigright promotion
owner of bigright boxing Gym
No comments:
Post a Comment