Na Salma Said
Wakati ambapo tume ye mabadiliko ya katiba inaendelea na mchakato wa upatikanaji wajumbe wa baraza la katiba nchini, wanasheria zanzibar wanasikitishwa na mgawanyiko na ushindani usiokuwa na tija uliojitokeza visiwani Zanzibar.
Wakizungumza katika kongamano la ‘kuadhimisha miaka 49 ya muungano na mchakato wa katiba,” wanasheria Othman Masoud Othman na Ali Uki walisema mgawanyiko unaojitokeza miongoni mwa Wazanzibari unasikitisha.
Othman ambaye ni mwanasheria mkuu wa Zanzibar alisema katika kongamano hilo lililotayarishwa na Chama cha wanasheria Zanzibar (ZLS) kuwa hatua ya ushiriki wa wananchi kwa upande wa Zanzibar katika mchakato wa kutafuta wajumbe wa mabaraza ulitawaliwa na fujo.
“Kwa maoni vangu ushiriki ulikua wa kuvunja rnovo sana kwa sababu zifuatazo. Kwanza ni ile va hatua hii kutawaliwa na itikadi za kisiasa, na hatimaye maoni arnbavo valihitaji Hoja vakawa kama kura arnbavo ilihitaji idadi. Wananchi walikubali kuwa watii kwa maslahi vao va itikadi za siasa badala va kuwa wapiganaji wa kupigania hatima vao, hatima va haki vao na hatima va nchi vao,” alisema Othman.
Aidha aliongeza kusema “sidhani kama tuliisaidia sana Tume ya katiba kwa sababu hatua hii ilitawaliwa, baadhi va sehemu, na jazba badala va hoja. Hatimave badala va mchakato huu kuwa wa kuimarisha umoja ukawa wa kutugawa, wa kutuletea uhasama na ugomvi; tofauti sana na muelekeo ambao tavari tulishauchukua katika nchi vetu.”
Akizungumzia muungano katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha taifa- Zanzibar (SUZA), mwanasheria mkuu alisema kuwa Muungano wetu umekuwa na matatizo mengi ambayo vanatishia kuvunjika kwake kama hayakufanyiwa mapitio va kina na dhati, na kurekebisha kasoro zake hasa zile ambazo ni za kiini.
Kwa mujibu wa Othman tafiti na taarifa kadhaa zimeonesha kuwa Muungano wetu una matatizo makubwa na ya msingi kabisa, “tuzitathmini kasoro hizo za msingi, tuzijadili kwa kina bila ya kuona haya au kuogopa taasisi zetu ama za itikadi au za itifaki. Tukifanya hivyo, kazi yetu katika Mabaraza ya Katiba itakuwa rahisi sana. Vyenginevyo, nina wasi wasi tutayageuza Mabaraza hayo kuwa ni maonyesho ya moja kwa moja ya Comedy za mfumo wa kizazi kipya.”
Othman amezitaja, baadhi ya kasoro za Muungano kuwa ni Misingi ya Muungano kutokuwekwa bayana; kukosekana usawa katika maamuzi vanavohusu mambo va Muungano; Kukosekana uwazi na usawa katika matumizi va rasilimali za Muungano; and mfumo wa sasa Serikali mbili ambapo wengi Wengi wanadhani kuwa mfumo wa sasa wa Serikali mbili unaweza kufanyiwa marekebisho na kuendelea kutumika.
Mwanasheria Ali Uki kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar (Zanzibar University) alizitaja baadhi ya changamoto za Mabaraza ya Katiba kuwa Tume kutoa muda usiotosha ukiliganisha na muda uliotolewa Kenya; Uwezo (capacity) ya kuchambua maudhui ya Rasimu ya Katiba; na kuwa demokrasia ya uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba imehojiwa.
Uki alisema kwamba Malalamiko huenda yakaathiri kukubalika Rasimu ya Katiba, an kwamba ni vigumu watu wa kawaida kufahamu madhumuni (intention) ya Rasimu ya Katiba kwa muda mfupi.
Washiriki wa kongamano hilo walikosoa uchaguzi wa kutafuta wajumbe wa mabaraza ya katiba na kusema kwamba haukupangwa vizuri na zaidi itikadi za kisiasa zilichukuwa nafasi kubwa kuliko kuchaguwa watu wenye uwezo.
No comments:
Post a Comment