Viongozi wanawake wa CUF wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fatma Ferej (wa nne kulia) katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika hoteli ya Bwawani.
Prof. Lipumba na Maalim Seif wakimpongeza Fatma Ferej kwa kupewa Tunzo ya mwanamke jasiri Tanzania kwa mwaka 2013.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Mhe. Fatma Ferej kwa kupewa tunzo ya mwanamke jasiri, 2013.
Viongozi wa CUF wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fatma Ferej (wa nne kulia) katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika hoteli ya Bwawani.
Viongozi wa CUF wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fatma Ferej (wa tatu kulia) katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika hoteli ya Bwawani
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Awena Sinani, akiangalia kazi za wajasiriamali wa CUF, akiongozana na Mhe. Fatma Ferej, katika hafla ya kumpongeza kutoana na kupewa tunzo ya mwanamke jasiri Tanzania 2013.
kwa picha zaidi bofya read more
kwa picha zaidi bofya read more
Wasanii wa ngoma ya Kingazija wakisubiri kutoa burudani katika hafla ya kumpongeza Fatma Ferej, hoteli ya Bwawani.
Wasanii wa ngoma ya Kingazija wakisubiri kutoa burudani katika hafla ya kumpongeza Fatma Ferej, hoteli ya Bwawani.
Mkurugenzi wa Fedha CUF Bi Zakia Omar, akimvisha koja Mhe. Fatma Ferej kama ishara ya kumpongeza kwa kupewa Tunzo ya mwanamke jasiri Tanzania, 2013.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Mhe. Fatma Ferej kwa kupewa tunzo ya mwanamke jasiri, 2013.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na viongozi wanawake wa CUF, katika shamrashamra za kumpongeza Fatma Ferej.
Akizungumza katika hafla maalum ya kumpongeza Mhe. Fatma Fereji kutokana na kupewa tunzo hiyo na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania tarehe 4/3/2013, Maalim Seif amesema Fatma Ferej ni mchapa kazi wa kweli na jasiri katika kutekeleza majukumu yake.
Amesema akiwa msaidizi wake katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais , Fatma Ferej amekuwa akimsaidia kwa karibu hasa katika kufuatilia masuala ya dawa za kulevya, mazingira na maendeleo ya watu wenye ulemavu.
Pia alimsifu kutokana na busara na mashirikiano yake na watendaji wengine wa Ofisi hiyo. “Sijawahi kupokea malalamiko kuwa Mhe. Fatma anawanyanyasa wafanyakazi wake, bali siku zote namuona ni kiongozi mwenye busara na mashirikiano makubwa”, alifahamisha Maalim Seif.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema Tunzo aliyoipata Fatma Ferej imekijengea sifa kubwa chama chake cha CUF.
Prof. Lipumba alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi na walezi kutowabagua watoto wao na kuwapa fursa sawa za kielimu ili waweze kujiandaa vyema kukabiliana na maisha, sambamba na kuwapa fursa wanawake waweze kushiriki shughuli za kijamii.
Nae Mhe. Fatma Ferej amesema anaichukulia tunzo hiyo kama ni changamoto ya kuzidi ari ya kiutendaji, na kuwataka wanawake wajiamini wanapotekeleza majukumu yao.
Amefahamisha kuwa wakati umefika kwa wanawake kuuthibitishia ulimwengu kuwa wanaweza, na kuondokana na mtazamo finyu kuwa kazi za wanawake ni kukaa jikoni pekee.
Hafla hiyo ya pongezi maalum iliyofanyika hoteli ya Bwawani, iliandaliwa na Jumuiya ya wanawake wa CUF.
Hassan Hamad, OMKR.
No comments:
Post a Comment