ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 5, 2013

Ubovu wa choo cha Shule

Katika utekelezaji wa kweli wa maendeleo ya Tanzania tunahitaji viongozi wachapakazi wenye moyo wa kutumikia wananchi na kukubali ushauri bila kujali nyadhfa zao. Bi.Fatma Said Ally ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino ni miongoni mwa viongozi ambao wanapongezwa na wananchi kutika juhudi zake za kuwa karibu na wananchi, taasisi pamoja na wadau katika Wilaya yake kwa lengo la kuwaletea maendeleo. MED inampongeza kiongozi huyu na kumtakia kila la kheri katika kutimiza azma yake ya kuifanya Wilaya ya Chamwino kuwa Wilaya zenye maendeleo chanya.(Pichani aliye simama ni mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi.Fatma Said Ally, kulia ni Bw. Baltazar Ngowi Afisa utumishi mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na kushoto ni Bw.Davis Makundi mratibu wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma.)(MED).
Hili ni jengo la choo cha Shule ya Msingi Ndebwe iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma choo ambacho wanafunzi hukitumia wawapo shuleni hapo.
Huu ni muonekano wa mbele wa choo hicho.
Hili ni moja ya tundu la choo hicho kinachotumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndebwe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Kiranja Mkuu wa Shule ya Msingi Ndebwe Iliopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,Rossemary Masaka. Haya ni moja ya mafanikio ya mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU,mradi ambao umeleta mapinduzi katika chaguzi mashuleni Wilayani Chamwino tofauti na zamani ambapo walimu ndio walikuwa wakiteuwa viongozi,jambo ambalo lilikuwa likiwanyima haki wanafunzi kuchagua viongozi wanaowataka. Hapa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndebwe walitumia Demokrasia kuchagua vingozi katika shule yao bila kujali jinsia.
Wanafunzi kutoka shule za msingi za,Mvumi misheni,Mvumi co,ed,Nyerere,Ilolo,Ndebwe,Mvumi makulu,,Chalula na Muungano. Wakifuatilia mafunzo juu ya chaguzi za Demokrasia na uundwaji wa mabaraza mashuleni,kutoka kwa maafisa wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma hawako pichani,ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU unaoendeshwa na shirika hili katika shule 14 za msingi na 6 za sekondari zilizopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, mradi ambao unafadhiliwa na OXFA GB.
Shirika la Marafiki wa Elimu Mkoani Dodoma pia hutumia vyombo vya habari kutoa Elimu kwa jamii kuhusiana, Elimu,Demokrasia na Utawala bora, kama inavyoonekana kwenye picha.
Mratibu wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma, Nd.Davis Makundi akiendesha mafunzo ya chaguzi za Demokrasia na uundwaji wa mabaraza katika shule 16 za msingi na 4 za sekondari zilizopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU unaoendeshwa na shirika hili kupitia ufadhili wa OXFAM GB

No comments: