ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 26, 2013

WAKATI MWINGINE WANAWAKE HUKOSEA BILA KUJUA!

KILA aliye kwenye uhusiano ana ndoto zake; wapo ambao wapo kwa ajili ya kupoteza muda, wengine wakiwa na nia ya kudumu na wenzi wao wakitegemea siku moja kufunga ndoa. Hawa ndiyo ninaozungumza nao katika mada hii.

Kama ni kweli upo katika uhusiano na unapenda kuishi na mpenzi wako siku za baadaye, lazima uwe makini katika kila unalolifanya, lengo likiwa ni kukuongezea pointi za kumfanya huyo akupendaye awaze zaidi juu ya kufunga ndoa na wewe.

Je, umewahi kujiuliza kwamba, kuna makosa ambayo wanawake huyafanya bila kujijua? Je, unafahamu kwamba, si kila kosa analofanya mwanamke hukusudia kukosea?
Yes! Marafiki zangu, wakati mwingine hutokea mwanamke akawa katika kuamini jambo fulani kuwa ni sahihi na akalifanya kumbe amekosea. Lengo la makala haya sasa ni kuwafumbua mambo wanawake wajue ni mambo gani ni makosa kwao kuyafanya ili kujenga uhusiano ulio bora zaidi.
Kwa kawaida huwa naandika kwa utafiti lakini kazi ya kupokea na kufanyia kazi hubaki mikononi mwa msomaji mwenyewe. Hebu twende tukaone...

KUMZIDI UJANJA MWANAUME
Wanaume wanapenda kupendwa kwa dhati, kama wakiwa wamependa kweli, nao huwa na msimamo sana. Lakini hakuna kosa kubwa ambalo mwanamke anaweza kulifanya kwa mwanaume kama kumuonesha kwamba yeye (huyo mwanume) hana ujanja kwake.

Amefika na hafurukuti kwa lolote. Fanya manjonjo yote lakini usijisahau. Kupendwa ni kawaida katika maisha, lakini kupendwa kwa mapenzi ya dhati ni bahati! Usicheze na bahati hiyo, kuwa makini na uoneshe mapenzi yako ya kweli, lakini siyo kumtishia au kufanya vituko vitakavyomfanya aone kabisa kwamba umemuona ‘wa kuja’ katika mapenzi. Umenisoma rafiki?

KUMNANGA X BOYFRIEND
Mwanaume anapokuwa na wewe, hakuna ubishi kwamba anatambua huko nyuma ulikuwa na uhusiano na wanaume wengine, vinginevyo awe ‘amekufungua kwenye makaratasi’ mwenyewe!

Lakini hii si tiketi ya wewe kuzungumza juu ya wanaume wako waliopita. Hakuna mwanaume anayependa kusikia habari za mpenzi wako wa nyuma, kwanza, anaumia. Ila kubwa zaidi anaanza kukufikiria kwamba wewe si mwanamke thabiti, kwani una msururu wa wanaume na yeye yupo kwenye historia ya cheni ndefu ya wanaume wako.

Kubwa zaidi, mwanaume anaamini kwamba, kutokana na kuzungumza kwako kuhusu wanaume waliopita (hasa kwa mabaya), siku akiachana na wewe atarajie kusemwa kwa mwenzi wako mpya, jambo ambalo hatapenda litokee.

Anapata nafasi ya kufikiria kuachana na wewe hasa kwa sababu umeshampa historia ya wanaume wengi hivyo kukuona mwanamke wa kupita tu na si wa kupanga mambo ya ndoa hapo baadaye.
Lazima atakuwa anawaza sana juu ya tabia yako hiyo ambayo kwake tayari itakuwa imeshakuwa tatizo. Unadhani atafanya nini ili aepukane na tatizo hilo? Unafikiri kuna njia nyingine kweli zaidi ya kuachana? Eti rafiki zangu, ipo kweli?...UTAACHWA HIVIHIVI!
Wiki ijayo tutaendelea na mada hii, SI YA KUKOSA!

No comments: