ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 3, 2013

Wakazi wa mabondeni Dar wakubali yaishe-Mwananchi

Kijana ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akiwa amesombwa na maji katika eneo la Mabibo Relini jijini Dar es Salaam jana, baada ya maji kufurika kutokana na mvua zinazoendelea. PICHA | Venance Nestory

Dar es salaam. Hatimaye baadhi ya wakazi wa mabondeni jijini Dar es salaam wamesalimu amri na kuanza kuyahama makazi yao kutokana na mfululizo wa matukio ya mafuriko katika maeneo wanayoishi.

Hatua hiyo imekuja baada ya mfululizo wa mvua zinazoendelea kunyesha nchini na kusababisha mafuriko katika maeneo ya mabondeni kwa kipindi hiki katika maeneo tofauti ya jiji huku maeneo ya Kigogo, Mabibo na Tandale yakiwa yameathirika zaidi.
Waandishi wa gazeti hili walitembelea eneo la Kigogo Mkwajuni na kushuhudia baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwa katika harakati za kuhama maeneo hayo.

Pia asilimia kubwa ya wakazi walikutwa wakiwa katika pilikapilika za kukausha vyombo vyao yakiwamo magodoro na kusafisha nyumba zao. Wakazi hao walisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na maisha ya wasiwasi, kwani tangu kuanza msimu wa mvua wamekuwa wakiishi kwa mashaka.

Khalid Hassan aliyekuwa akipakia mizigo yake ndani ya gari tayari kuhama eneo hilo alisema alikuwa na mpango huo tangu awali, lakini alikwamishwa.

No comments: