ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 28, 2013

WATANZANIA NEW YORK WASHEREKEA SHEREHE ZA MUUNGANO KWA MAFANIKIO

Mh.Balozi Ramadhan Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilizofanyika jijini New York. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watanzania wengi kutoka katika miji ya jirani ya New York kama New Jersey, Delaware, Massachusetts na Connecticut. 
Watanzania waliungana kwa pamoja kwa kula chakula na kucheza muziki sambamba na vinywaji baridi.
Katibu wa Jumuiya ya watanzania New York Bwana Shaban Mseba akisoma risala katika sherehe  za muungano
Mwenyekiti wa jumuiya Hajji Khamis akiongea machache mbele ya watanzania waliojitokeza katika sherehe hizo zilizofanyika New York katika kitongoji cha New Rochelle.
Dr Chemponda alikuwepo kuongea machache juu ya jinsi gani anavyoujua muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mama Ashura Duale nae anaujua sana muungano wa Tanganyika na Zanzibar na alikuwa mmoja ya washuhuda wa uchanganyaji mchanga wa pande zote mbili za Tanganyika na Zanzibar
Hii ndiyo cake ya muungano ikiwa mezani
Ukodak wa pamoja kutoka kushoto ni Dr Chemponda, mama Ashura ambaye ni mama mwenye nyumba wa Mh. Balozi Mwinyi, na Mh. Balozi Mwinyi
Ukodak mbele ya cake 
Mh. Balozi akikata Cake tayari kwa kuwalisha wana muungano waliofika katika sherehe hiyo
Mh. Balozi Ramadhani Mwinyi akimlisha kipande cha cake mama mwenye nyumba wake kabla ya watu wengine hawajapata nafasi hiyo. 
Kwa picha zaidi ya sherehe hizo zilizofanyika katika jiji la New york bofya read more.


No comments: