Zaidi ya watu milioni 33 wakiwemo watoto wenye umri wa chini ya mika 18 wameambukizwa virusi vya vinavyo sababisha ugonjwa wa ukimwi (VVU) duniani.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2010 na shirika la Unaids,
Idadi hiyo ya watu wanaishi na virusi vya ugonjwa huo duniani.
Aidha, utafiti uliofanywa mwaka 2008 ulibaini kuwa, zaidi ya watu milioni 1.2 wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ambao idadi yao ni sawa na asilimia tano ya watu wazima, wanaishi na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi.
Akitoa mada kuhusu ajira za watoto migodini na maambukizi ya VVU kwa wanawake na athari zake, katika semina ya
siku mbili kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika mjini
Shinyanga, Mkurugenzi Msaidizi Utawala wa Wizara ya Nishati na
Madini, Suleiman Mvunye, alisema nusu ya waathirika ni wanawake.
Alisema utafiti uliofanywa nchini mwaka 2009, ulionyesha kuongezeka kwa maambukizi mapya ambayo yalionyesha kufikia watu 100,000 ambao ni sawa na watu 275 waliokuwa wakiambukizwa virusi vinavyosababisha ukimwi kila siku.
Mvunye alisema asilimia 60 ya wanawake wameabikizwa virusi
vinavyo sababishwa ugonjwa huo kutokana na sababu kuu ya maumbile yao, ikiwa ni pamoja na sababu nyingine mbalimbali na kufanya kuongezeka kwa maambukizi kwa wanawake hadi kufikia asilimia 75.
“Zaidi ya watu 86, 000 walikufa mwaka 2009 kutokana na magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na ukimwi na idadi kubwa ya watu hao ni kutoka vijijini ambako taarifa zao hupatikana kwa shida” aliongeza kusema.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment