Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimshukuru Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose kutokana na ubalozi huo kutoa mafunzo ya mitandao ya kijamii (Social Media) kwa maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zake yaliyofanyika mwezi wa tatu mwaka huu. Balozi huyo alimtembelea waziri Dk. Mukangara ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kuimarisha mahusiano baina ya Wizara hiyo na Uingereza.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiongea jambo na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Balozi huyo aliahidi kuendelea kushirikiana na wizara hiyo katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na kuendelea kutoa mafunzo kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akisalimiana na Joseph Paync ambaye ni afisa miradi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akibadilishana kadi ya mawasiliano (Business Card) na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Ubalozi wa Uingereza umeahidi kushirikiana na wizara hiyo katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na kuendelea kutoa mafunzo kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
(Picha na Anna Nkinda – Maelezo)
No comments:
Post a Comment