Wenza ambao mmoja wao ana Ukimwi, wanatakiwa wapate ushauri na wazingatie kinga wakati wa tendo la ndoa mara baada ya mmoja wao kugundulika kuwa na maambukizi
Umeshawahi kusikia matukio ya kuwepo kwa wanandoa au wenza ambao wameishi kwa muda mrefu wakishiriki tendo la ndoa, lakini mmoja anapata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na mwingine hana?
Wenza wa aina hiyo wanaitwa kwa lugha ya Kiingereza ‘Discordant Couple’
Wenza hao, huweza kupata watoto kadhaa lakini bado mmoja wao akawa hana maambukizi. Kwa kawaida, wenza wa aina hii ambao huwa hawapati maambukizi ni wanaume.
Mwaka 2008, utafiti ulifanyika na kugundua kuwa asilimia 40 hadi 50 ya wanandoa, mmoja wao hana maambukizi(Bunnel na P.Cherutich: 2008)

Mwaka 2006 Benki ya Dunia ilifanya utafiti kuhusu wenza wa aina hiyo katika nchi za Tanzania, Burkina Faso, Ghana na Kenya.
Ilibainika kuwa robo tatu ya watu wenye VVU wana wenza wasio na VVU.
Kilichobainika zaidi ni kuwa asilimia 30 hadi 40 ya wenza wa aina hiyo, wanawake ndiyo walikuwa wameathirika.
Daktari wa Uchunguzi wa Magonjwa katika hospitali ya Muhimbili, Innocent Mosha anasema aghalabu katika wenza wa aina hii, wanawake ndiyo huwa na maambukizi.
“Ni kesi chache mno, hakuna kesi ambayo mwanamume anakuwa na maambukizi,mara nyingi wanawake ndiyo huwa na VVU” anasema

Anasema maumbile ya mwanaume humsaidia asipate maambukizi endapo hatasababisha michubuko.
Kwa nini hawakuambukizwa?
Wataalamu wa afya wanasema, kutokana na aina ya maumbile ya mwanaume, wakati mwingine ni vigumu kupata maambukizi kwa sababu pengine hakupata michubuko wakati wa tendo hilo.
Lakini pia, inawezekana wanamume wa aina hiyo wana kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi au chembechembe zao za kinga hazina mapokezi au receptors vya virusi vya Ukimwi.

Virusi vya Ukimwi huweza kuingia kwenye chembechembe za kinga kupitia vipokezi mithili ya ufunguo na kitasa au nati na boriti.
Dk Mathew Dolan, wa Jeshi la Anga la Marekani, anasema uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU wakati mwingine ni wa kurithi na huweza kutokea kwa njia mbalimbali na katika makundi mbalimbali ya kikabila.
Kwa mfano, watu wa Bara la Ulaya na Asia ya Kati miili yao ina uwezo wa kujikinga na maradhi hayo.
Mfamasia katika hospitali ya Amana, Christopher Masika, ambaye yupo katika kitengo cha kuhudumia watu wenye VVU anasema wapo wenza wa aina hiyo kwa wingi hapa nchini.
Anasema wanapofika katika kitengo chake, wanaelekezwa namna ya kuishi na kubadili mtindo wa maisha.

“Ni lazima wabadili mtindo wa maisha, lazima wawe waaminifu na watumie kinga” anasema Masika
Anasema mmoja wa wenza hao kukosa maambukizi ya VVU, si kigezo cha kuwa salama bali wanahitaji kuchukua tahadhari.
Anasema: “Iwapo watahitaji kupata mtoto, basi ni lazima mwanamke apime ukubwa wa CD4 zake”
Kwa nini wanawake huathirika zaidi?
Mfamasia Masika anasema katika wenza wa aina hii, kwa kawaida wanawake huwa ndiyo waathirika kwa sababu ya maumbile yao.
“Pengine wenza hao awali, walikuwa wote hawana maambukizi, lakini mwanamke akaupata ama wakati akiuguza au katika ajali, lakini mwenza wake asiambukizwe” anasema
Masika anasema kuambukizwa kwa kawaida inategemea aina ya ufanyaji wa mapenzi.
Kwa mfano, mwanamke akiandaliwa vyema kabla ya tendo la ndoa na kisha isiwepo michubuko basi mwanamume anaweza asipate maambukizi.

“Ni vyema mwanamke akitayarishwa vizuri, kingine kinachosababisha virusi kuingia kwa urahisi ni vidonda wakati wa msuguano” anasema
Masika anasema mwaka 2007,ulifanyika utafiti na kubainika kuwa wapo watu wenye ‘CD4 receptors.’
Anasema watu hao, ni vigumu kwa virusi vya Ukimwi kupenya na kushambulia mwili.

“Ili kirusi kifanye kazi katika mwili ni lazima kinase katika cd4 receptors ambayo hushambuliwa na kusababisha kinga ya mwili kushuka” anasema
Iwapo mtu hana mirija ya mapokezi katika kinga yake, vijidudu hivyo hukosa chakula na hupotea.

“Kirusi kikikosa ushirikiano na chakula, kitakaa na mwishowe kitakufa chenyewe, kwa hiyo mtu huyo akipimwa hawezi kukutwa na maambukizi” anasema
Chimaraoke Izugbara, Mtafiti wa Afya na Idadi ya Watu Afrika anasema ipo haja ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wenza wa aina hii, hasa wanaume.

Anasema kwa kawaida wanawake ndiyo hufahamu na kuelimishwa kuhusu uzazi wa mpango huku wanaume wakiwa hawajui lolote.
“Linapokuja suala la mwenza mmoja ana VVU, basi ni lazima mwanaume aelimishwe” anasema

Anasema jamii imeagamia upande mmoja ambapo wanaume hawataki wala kujihusisha kuhusu uzazi wa mpango na wake zao hivyo hawawezi kufanya jitihada ya kupata huduma hizo.
“Wengine wanadhani mwenza wako akiwa anatumia ARV basi upo salama hata usipotumia kinga. Ipo haja ya kutoe elimu ili kuondoa dhana hizi” anasema Izugbara

Changamoto
Katika mahusiano ya aina hii, wenza hukosa furaha ya tendo la ndoa
Ugomvi na malumbano yanaweza kutokea iwapo wawili hawatapata elimu ya kutosha.
Vilevile, wanaume wengi huwakimbia wake zao pindi wanapogundulika kuwa na VVU na wao hawana.

WHO
Aprili 18 mwaka jana, Shirika la Afya Duniani lilitoa mwongozo kwa wenza wa aina hii duniani.
WHO lilisema kuwa wenza hao wanatakiwa kupewa ushauri mara kwa mara juu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi katika mahusiano hayo.
Pamoja na miongozo mingine WHO ilisisitiza wenza hao kupimwa na yule mwenye VVU aanze kutumia dawa na asiye na VVU pia, anywe dawa za kuzuia maambukizi.

Ushauri
Kutokupima Ukimwi kwa muda mrefu huku ukiendelea na kufanya tendo la ndoa.
Wanandoa hawana budi kuhakikisha wanafuata masharti ya kinga ili wasipate maambukizi.

Mtoto anayezaliwa na mama au wazazi wenye Ukimwi si lazima awe ana fuata ushauri wa daktari na hasa kupima wakati wa ujauzito
Tuangalie namna ya kuwadhibiti waganga wa jadi na wale wanaoshauri watu wasitumie dawa za kuongeza maisha.

Mwananchi
1 comment:
Kumkimbia mwenzio akiwa na VVU au kumsimanga ni makosa sana,kwa mfano umegudua mume/mke wako wa ndoa ana VVU halafu ukamkimbia kisa ana VVU!!hivi unakumbilia wapi?hujui kuwa ulipo hapo ni salama zaidi kwakua tayari unalijua tatizo ni nyinyi tu wenyewe kukabiliana nalo na mapenzi kama kawaida,sasa huko unakokimbilia hupajui je unauhakika na huko ni salama? mwishowe utakuja kuend up na kile ulichokikimbia na saa nynginee kuwa wors kuloko hata kwa mwenzio uliemkimbia,anyway hayo ni maoni yangui tu.
Post a Comment