Friday, May 24, 2013

Africa Day 2013-Golden Jubilee Gala Dinner yafana

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Lily Munanka mbaye amewakilisha Nchini ya Tanzania katika  Tamasha la Africa Day 2013 lililofanyika Alhamisi Mei 23, 2013 ndani ya Ukumbi wa Hilton Hotel Jijini Washington Dc
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani  na Mexico Mhe.Lily Munanka , na mwakilishi wake waliingia kwenye ukumbi kufuatana na alfabeti za Nchi wanazowakilisha. Tanzania ilitajwa namba 20, Lily Munanka  akisindikizwa na Mwana Mitindo mbunifu wa (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Lily Munanka walipokua wakingia ndani ya  ukumbi wa Tamasha   la Africa Day 2013-Golden Jubilee Gala Dinner Siku ya Alhamis Mei 23,2013 ndani ya Ukumbi wa Hilton Hotel  uliopo Connecticut Ave, Jijini  Washington Dc
Kaimu Balozi wa Tanzania Mama  Lily Munanka na Mshika Bendera ya Tanzania Missy Temeke wakielekea sehemu ya mapokezi  ili kuwakilisha rasmi  Nchi ya Tanzania katika tamasha la Siku ya Afrika 2013 (Golden Jubilee Gala Dinner) Siku ya Alhamis Mei 23,2013 ndani ya Ukumbi wa Hilton Hotel uliopo Connecticut Ave, Jijini  Washington Dc
Kama taratibu za sherehe hizo zilivyoandaliwa, mabalozi wote 50 waliingia ukumbini wakiwa wamependeza kabisa na baadhi yao waliovalia Mavazi ya kiAfrika huku wakiwa wameshikilia bendera zakuwakilisha nchi zao kitaifa, Miongoni mwa warembo alikuwepo Mwana Mitindo wa (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani  na Mexico Mhe.Lily Munanka, akiwa na baadhi ya maafisa wa ubalozi wakati wimbo wa taifa ulipokua ukipigwa.
  
Ofisa wa Balozi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Suleiman Saleh akiwa na Edward Taji kushoto kwenye Tamasha la Africa Day 2013-Golden Jubilee Gala Dinner Siku ya Alhamis Mei 23, 2013 ndani ya Ukumbi wa Hilton Hotel Jijini Washington Dc
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly kiwa na Abdul (katikati) pamoja na Mwana Mitindo mbunifu wa (Kwetu Fashion Design) Missy Temeke

Mamia ya wageni kutoka mataifa mbali mbali waliojumuika rasmi kwa ajili ya Tamasha la Siku ya Afrika 2013 (Golden Jubilee Gala Dinner) Siku ya Alhamis Mei 23,2013 ndani ya Ukumbi wa Hilton Hotel uliopo Connecticut Ave, Jijini  Washington Dc

Mkuu wa UNICEF, na pia aliekua mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu Nchini Marekani NBA kutoka JKK, Dikembe Mutombo, akiwa  kwenye African Day 2013 anayofanyika kila mwaka May 23, 2013 Jijini Washington DC

Balozi wa Kenya nchini Marekani, Mhe. Elkanah Odembo, akitoa Hotuba kwenye Tamasha la Africa Day 2013-Golden Jubilee Gala Dinner Siku ya Alhamis Mei 23,2013 ndani ya Ukumbi wa Hilton Hotel Jijini Washington Dc
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Lily Munanka wapili toka kulia, akipata picha ya pamoja na waTanzania waliohudhuria katika Tamasha la Siku ya Afrika 2013 (Golden Jubilee Gala Dinner). Kwa picha zaidi bofya read more


Picha kwa hisani ya Swahili Villa Blog

No comments: