Uongozi wa klabu ya Azam inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara umesema kwamba hawatakuwa na wachezaji wapya katika kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na kuzitaka timu nyingine kutokuwa na hofu ya kuchukuliwa nyota zao kama inavyozungumzwa katika kipindi hiki cha usajili.
Wachezaji ambao wamehusishwa kutaka kujiunga na Azam ni pamoja na Shomary Kapombe na Juma Kaseja wote kutoka Simba.
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor, alisema kwamba kikosi chao kiko imara na wanachokifanya ni kupandisha wachezaji kutoka timu B wakati wale wasiokuwa na nafasi watapelekwa kwa mkopo katika timu nyingine.
Nassor alisema kwamba wachezaji wengine wamekuwa wakidanganya kutaka kusajiliwa na Azam kwa malengo ya kutaka 'kujipandishia' dau kwenye timu zao, huku kukiwa na uvumi kwamba wao wamedhamiria kusajili nyota wapya wakiwamo kutoka Simba na Yanga.
Aliongeza kuwa wataanza msimu ujao wakiwa na nyota wao walioitumikia klabu hiyo msimu huu na kumaliza ligi wakiwa kwenye nafasi ya pili na endapo wataona wanahitaji kuongeza nguvu, itakuwa ni Novemba katika kipindi cha dirisha dogo la usajili.
"Hatutakuwa na sura mpya kwa sasa katika kikosi chetu, ikibidi kufanya hivyo ni hadi kipindi cha dirisha dogo mwezi Novemba na hapo tutaangalia zaidi wa kutusaidia katika Kombe la Shirikisho," alisema Nassor.
Alisema kwamba kwa sasa uongozi unaendelea na mipango ya kuandaa ziara ya nje ya nchi kwa timu hiyo kama ilivyofanya kwa miaka miwili iliyopita na mazoezi rasmi yatafanyika kuanzia Juni 24 asubuhi kwenye uwanja wao wa Azam Complex.
Mwaka jana timu ya Azam ilienda katika nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo ilicheza mechi mbalimbali za kimataifa za kirafiki.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment