Hali ilivyokuwa kanisani hapo juzi. |
DEREVA wa pikipiki maarufu kama bodaboda, Victor Ambrose, anatuhumiwa kurusha bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu wawili na wengine karibu 70 kujeruhiwa.
Ambrose mwenye umri wa miaka 20 na mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha, anashikiliwa pamoja na watuhumiwa wengine tisa, wakiwemo raia wanne wa Saudi Arabia kwa mahojiano zaidi ya kuhusika na tukio hilo.
Taarifa zilizopatikana jana jioni, zilieleza kuwa raia hao wa Saudi Arabia, waliingia nchini Jumamosi usiku kwa ndege kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na baada ya tukio Jumapili, waliondoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga.
Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, ilitoa taarifa hiyo jana bungeni na kueleza namna uhalifu huo ulivyotendeka kanisani hapo juzi, muda mfupi baada ya ibada kuanza.
Kwa mujibu wa Waziri Nchimbi, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Hata hivyo uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika, unaendelea kufanywa na Polisi na wataalamu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
“Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Miongoni mwao ni Victor Ambrose mwenye umri wa miaka 20 dereva wa bodaboda...ambaye anatuhumiwa kurusha bomu hilo. “Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa mahojiano,” alisema Dk Nchimbi.
Waziri alitaja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni mtoto mwenye umri wa miaka 16, James Gabriel, aliyefariki usiku wa jana na Regina Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariki siku ya tukio wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema waliokamatwa wamefikia 10, na raia hao wa nje ni wa Saudi Arabia.
Alisema pia mtu wa tatu alifariki lakini hakumtaja jina. Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Dk Mariam Murktadha, alifafanua kuwa kijana Gabriel, alifia Uwanja wa Ndege wa Arusha, akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Aliongeza kuwa majeruhi walikuwa 66 na hivi sasa wamebaki 34 na wengine wameruhusiwa.
Kwa mujibu wa Dk Nchimbi, majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Mount Meru, wengine Hospitali ya St Elizabeth kwa Father Babu, Hospitali ya Selian na mwingine alipelekwa katika Hospitali ya Dk Wanjara, Mianzini.
Bomu lilivyorushwa
Akielezea tukio hilo, Waziri Nchimbi alisema lilirushwa wakati mgeni rasmi, Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Padilla, akiwa ametoka nje ya kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi.
Alisema mtu huyo alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi, kwenda eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu na baada ya kutua, kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa. Inakadiriwa uzinduzi huo wa Kanisa, ulihudhuriwa na watu zaidi ya 2,000.
Alisema viongozi wa dini na Serikali waliohudhuria ibada hiyo, hawakupata madhara yoyote kutokana mlipuko huo. Udini Amewasihi Watanzania kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiwasaka walihusika na shambulio hilo.
Aidha ametaka kila mwenye taarifa za kuwezesha kukamatwa wahalifu hao azitoe Polisi. Kwa mujibu wa Waziri Nchimbi, siku za hivi karibuni kumekuwepo jitihada kubwa za watu wachache wasioitakia mema nchi, kutaka kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kuleta mapigano na mauaji.
“Sina shaka kuwa shambulio la Arusha ni sehemu ya mikakati hiyo miovu,” alisema bungeni na kusisitiza kwamba Serikali itachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii.
Wanasiasa waonywa
Wakati huo huo, Waziri Nchimbi amekemea wanasiasa wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kupitia tukio hilo, akisisitiza kwamba Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheria itakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hiyo.
“Kokote duniani tukio la kushitukiza linalosikitisha na kuhuzunisha kama hili linapotokea, wananchi wote huungana na kuwa wamoja kama taifa na kulaani wahusika na kuwafariji waathirika wa tukio hilo,” alisema Dk Nchimbi.
Akikemea wanasiasa wanaotumia matukio kujinufaisha, huku akitoa mfano wa Marekani na kusema mgombea mmoja wa urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2012, aliishutumu Serikali kutokana na kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani nchini Libya.
“Ni wazi kuwa mgombea huyo alichukua tatizo lile kama ajenda ya kisiasa. Hata hivyo alishutumiwa vikali na Wamarekani wenzake kwa kuelezwa kuwa ni mtu mwenye kukosa kabisa misingi ya uaminifu na uzalendo kwa taifa lake.”
“Serikali inasikitishwa sana na wanasiasa wa aina hii, ambao wanajitokeza nchini na kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa gharama za maisha ya Watanzania…Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheria itakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hii, ambao maslahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania,” alisema.
Dk Nchimbi alilaani waliohusika kufanya uhalifu huo na kusema Serikali kwa nguvu zote itahakikisha watuhumiwa wote waliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hilo, wanasakwa popote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
“Tunawataka viongozi wa kisiasa, kidini na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika, ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu,” alisema.
Imeandikwa na Stella Nyemenohi, Dodoma na Veronica Mheta, Arusha.
Source: Habari leo
10 comments:
nilijua kambwa watasingiziwa waislamu ndo mwimba unaowachoma moyoni na mungu kishasema daima dini yake hatotoweka eti wasaudi halafu unambiwa aliye rusha bomuni mkiristo aliye wachomea watu
lakin mungu mkubwa fanyeni mnayoyafanya mkae mkijua mkono wa mungu ukikufikiyeni ndo mtamjua
kila leo eti mnaripuliwa nyinyi kwani nyinyi nani mnajiripuwa wenyewe ili mpata ruzuku serikalini na halafu kujitaba kwamba dini yenu ndo njema haina magaidi
na usiweke comment hizi najua hutoziweka lakini utakuwa umeshasoma ujuwe kwamba watanzania wakiislamu si wajinga
nilijua watakuja na gia hii wanajirupuwa wenyewe kama maju wafanyavyoo lakini uislamu hatodidimia hata mkiupata chuki yeyote ile and its a true religion haina propaganda kama zenu za mabwana wenu wakizungu
shabash nilijua watasema haya so si siri wala si jambo geni kila tukio lazima watajidai magaidi wa saudia
watu tupo macho babaaa, maaaamaaaa
alivyoulizwa jamaa huyu aliyeripuwa na kuwachomeya hawa masaudian kisa kupaka tope uislamu nataka kuuliza hivi alirikodiwa na tuwekeni hii clips
mwanasheria aliyekubuhu na bado nasoma sheria kwa undani na jinsi alili za binadamu zinavyotumia propaganda ili kujiunga mkono na ile maada wanayo taka kuitoa
Wewe anon wa 7:09 pm unajua unachokiongea? Kwani huwezi ukajiita jina la kikristu ili usijulikane? Najua watu wengi tu wanaitwa david, joseph nk lakini ni waislaam au wanatumia majina ambayo si yao. Nchi yenyewe hiyo haina vitambulisho kufoji jina rahisi (Tusubiri uchunguzi, tuone kama hao ni dini gani?), Unaongea usilojua nani kakuhakikishia kuwa uislaam ni dini ya ukweli? na unasema ukristo ni dini ya mabwana zenu wa kizungu, kwani huo uislaam ulianzia Rufiji au Kisarawe? Kama huelewi, uislaam walianzisha waarabu. Kwa hiyo wote wazungu na waarabu wote walituletea dini zao, hizi ni dini za mapokeo tu tuliyoletewa na wala hatuna uhakika kuwa ipi ni kweli au ipi ni uongo.
Pole huyo anonymous wa 7.09 pm hajaenda shule si makosa Yake msamehe tu.
Jamani tutumie akili japo kidogo tu, kwanini huyo dereva wa boda boda yeye jina lake linafahamika lakini la raia wa Saudi Arabia majina hakuna ilihali walikuwa na hati za kusafiria? Je huyu dereva ni yeye kweli au usafiri wake ndio ulikuwa umembeba mtuhumiwa? Je mtuhumiwa hasa ni nani? Je huyu dereva kweli jina lake ni Victor? Je huyu dereva ametumwa na nani hasa? Je hayuko kwenye mtandao na watanzania wengine waliopanga hilo au yeye alikuwa tu na wa-Saudi? Something is missing here or otherwise the whole thing is not true. Mtuhumiwa halisi might still be outthere.
Wakatoliki ni tabia yetu ya kuwapenda maaadui zetu siku zote na kuwapa huduma muhimu za kijamii kama elimu, hospitali, maji safi nk. Anayetudhuru kwa chochote sisi humuembea kwa Mungu kwa sababu tunaamini kuwa hata maadui zetu wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu mwenyewe anayetuambia "wapendeni adui zenu"
Mimi nadhani marumbano ya nani na ni wadini gani aliyefanya uharami kwa raia wa Tanzania wasio na hatia. Kweli tatizo limetokea tuwe macho ktk kuangalia kusiwe na machafuko. Kila mtanzania awe kama askari wa kulinda amani kwa njia yeyote ya kawaida. Kuonyeshana vidole ktk mtafaruku, hususani wa kigaidi kama huu wa kupoteza maisha na kubadili maisha ya watu kwa kujeruhiwa. Tushikamane kulinda taifa letu.
Mdau wa washington.
Huhitaji kuwa na akili ziada kuelewa kuwa, jina si hoja.
Pili, ili kuficha ukweli, ni rahisi mwislamu wa Saudia au UAE au Tanzania kumhonga hela kijana mkristo maskini na kisha kumpa bomu afanyizie ili baadaye watu washindwe kuupata ukweli.
Lakini, kiushahidi, na kimafundisho, na kiuzoefu, binadamu wote wanajua ni dini gani inaendekeza mambo ya mashambulizi na mauaji kwa kulitumia jina la Mungu. Kila mtu anajua hapa duniani na wenyewe tunajijua.
Tanzania yetu imeingiliwa. Redio Imani ya Morogoro inahubiri chuki na waislamu tumekaa kimya tu. Gazeti la Al Nuur linahubiri chuki na siye tuko kimya tu. CD na DVD za akina Sheikh Ilunga zinahubiri chuki na mauaji tunachekelea tu. Makanisa zaiid 40 yameshachomwa katika miaka miwili tu. Padri na mchungaji wameshauawa na watu wanaojulikana vema kabisa. Yule shehe wa Zanzibar aliuawa na sisi Waislamu wenyewe kutkana na msimamo wake. Bucha za nguruwe zilivunjwa miaka ile. Tunataka ushahidi gani zaidi?
Kuna mkristo gani ametuchokoza? Hata serikali inatubeba sana tu hadi imetupa chuo kikuu cha bure.
Tukio la Arusha lina harufu yote ya ugaidi wa kidini na sitashangaa kama ni sisi waislamu. Tuache kuukwepa ukweli. Waislamu na Wakristo na wengineo wa Tanzania tuweni waangalifu; la sivyo tutaumia.
Maneno ya mihadhara na huyu ustaadhi hapo juu si ya kweli. Wakristo wanajitegemea kwa sadaka na ndiyo maana wana hivyo walivyo navyo. Waislamu ni mpaka atokee mhisani wa Uarabuni, hatuwezi kujilinganisha. Wakristo wanatusomeshea watoto zetu, wanatuzalishia wake zetu, na wanatufanyia operesheni mabusha yetu kwenye hospitali zetu, tuacheni kuwachukia. Tujengeni vyetu. Bila ruzuku ile hakuna mwislamu atakayemudu gharama za matibabu Bugando na KCMC - tusemeni ukweli.
Wabilah Tawfiq.
Post a Comment