ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 8, 2013

GUNINITA AWASHUKIA MAOFISA ARDHI -ASHANGAZWA NA UJENZI NDANI YA HIFADHI

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Ilole Kilolo, alipofika kutatua mgogolo wa ardhi unaowakabili wananchi wa kijiji hicho na kijiji cha Ilambilole kilichopo Wilaya ya Iringa.
"Tunakuelewa mkuu," Ni kama wanasema wananchi hawa. 
Wananchi wa kijiji cha Ilole wakimsikiliza mkuu wa Wilaya hiyo Gerlad Guninita katika mkutano wa hadhara, kijijini hapo. 
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita akiwa katika eneo lenye mgogolo, baada ya kufunga safari hadi katika eneo lenye mgogolo ili kufanya suluhu ya tatizo hilo, akiongozana na kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kilolo na wananchi, pamoja na uongozi mzima wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. 
Askari polisi wakiwa katika eneo hilo lenye mgogolo, baada ya mkuu huyo wa Wilaya ya Kilolo kuamua kufika hadi katika eneo husika.
Nyumba iliyojengwa ndani ya eneo la marisho ya mifugo.
Retisia Kayuyuva mkazi wa kitongoji cha Igominyi Ilole Wilayani Kilolo, akimuonyesha mwanajeshi jani la mboga aina ya "MTOSI" ambao hutumia sana wakazi wa eneo hilo.

MKUU wa wilaya ya kilolo Gerlad Guninita amesema migogolo mingi ya ardhi, inatokana na baadhi ya watumishi wa idara hiyo kutanguliza mbele maslahi yao binafsi na hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Guninita ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa utatuzi wa mgogolo wa ardhi, baina ya kijiji cha Ilambilole kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kijiji cha Ilole kilichopo katika Wilaya ya Kilolo, ambapo naye mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Retisia Warioba alishiriki ili kutafuta suluhu ya tofauti hiyo.

Mkuu huyo amesema baadhi ya wataalamu wa ardhi ni tatizo na chanzo kikubwa cha uwepo wa migogolo baina ya wakulima na wafugaji, na hivyo kuipa shida serikali juu ya utatuzi wa pande hizo mbili zinapokinzana, huku akishuhudia ujenzi wa nyumba ndani ya hifadhi ya ardhi iliyotengwa kwa ajili ya malisho.

“Niwaeleze ukweli hapa kuna kila hila mbaya imetendeka, mjue nyinyi mmesomeshwa kwa kodi za watanzania hawa ili muwahudumie ipsavyo na sio kuwababaisha!!, Lakini kwa jinsi inavyoonekana hapa kuna hila ilifanyika,” Alisema Guninita.

Aidha alisema kazi ya wataalamu ni kutoa ushauri mzuri ili kuwaelimisha wananchi na hivyo kupunguza migogolo, huku akishangazwa na namna ya utatuzi wa mgogoro huo baina ya kijiji cha Ilambilole na Ilole ambapo ardhi ya ukoo wa Nyakunga imebadilishwa matumizi pasipo wahusika kushirikishwa.

“Ni kweli tunahitaji mifugo kwa ajili ya Nyama na Maziwa, lakini pia tunahitaji Kilimo kwa ajili ya chakula, lakini kama mtalamu badala ya kutumia elimu yake kumaliza tatizo linalowakabiri wananchi unageuka kuwa ndiyo chanzo cha tatizo kwa kuwa Beas (Guegemea upande mmoja) lazima uzalishe mgogolo mkubwa,” Alisema Guninita.

Pia alisema hakuna serikali itakayovumilia watendaji wa aina hiyo, ambao wanatumia utaalamu wao kuwadhurumu wananchi, na hivyo kuwataka wataalamu wa idara ya ardhi kuhakikisha wanatenda haki kwa wamiliki halali wa eneo hilo.

“Tukubaliane hapa,!! Hawa akina Nyakunga wanatakiwa wapate haki yao ya ardhi, ninahitaji wananchi waishi kwa amani na utulivu kwa kumaliza mgogolo huu,” Alisema.

Ibrahimu Kiteve mkazi wa kijiji cha Ilole alisema kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazao, kutokana na mgogolo uliopo baina ya wafugaji wa jamii ya Wamasai ambao hulisha mazao mifugo yao.

Kiteve alisema wamepata vipigo baada ya kulalamikia mazao yao kuliwa na Ng’ombe wa wamasai hao, na hali hiyo inatokana na baadhi ya wananchi kuwekezewa mifugo na wafugaji hao ambao wanamiliki idadi kubwa ya mifugo.

“Wakuu hapa nilipo siwezi hata kufanya kazi za kutumia nguvu baada ya kupigwa na wamasai nilipolalamikia Ng’ombe zao kuingiza katika shamba langu, hili ni tatizo kubwa sana hapa kijijini tunaombeni mtusaidie,” Alisema Kiteve.

Ombeni Ngwenga alisema tatizo hilo mwaka jana lilisababisha mapigano ambapo jeshi la polisi lilifika kuingilia kati, baada ya wakulima nao kuchoshwa na tabia ya Ng’ombe kuingizwa katika mashamba yao.

Wananchi hao walisema licha ya mgogolo wa pande hizo mbili, lakini wingi wa mifugo unachangia uharibifu wa mazingira, huku wakishangazwa na tabia ya watumishi hao wa serikali kuzuia shughuli za kilimo kwa wamiliki halali wa ardhi hiyo, huku mfugaji huyo mwenye jamii ya Kimasai akiruhusiwa shughuli za ufugaji na hata kujenga nyumba katika eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho.

Hata hivyo mkuu huyo aliwaagiza viongozi wa kijiji cha Ilole kutoa amri kwa wananchi kurudisha mara moja mifugo kwa mmiliki halali, kwa madai ya kuwa kijiji hicho hakina uwezo wa kuwa na idadi kubwa hiyo ya mifugo.

1 comment:

Anonymous said...

Na sitachoka kukosoa
Mgogolo , umechemsha!
Kiswahili fasaha:- MGOGORO.