Friday, May 17, 2013

HUSNA AKANA KUWA NA MAHUSIANO NA MWANA F.A

MISS Sinza 2011, Husna Maulid, juzikati ameibuka na kudai kwamba katika maisha yake hajawahi kutoa penzi kwa msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’. Husna aliyasema hayo Mei 15 mwaka huu baada ya kuvumishiwa kuwa anatoka kimapenzi na staa huyo na kwamba, kwa sasa hakuna kificho chochote kwani hadi picha zinazowaonyesha ukaribu wao zimezagaa kwenye mtandao.“Sijawahi kutoka na Mwana FA, zaidi ya kufanya naye tangazo ambalo niliombwa na dada’ngu, Mboni Masimba nikafanye naye kwa ajili ya shoo ambayo anaiandaa hivi karibuni, wanaonihusisha na mapenzi na Mwana FA hawanitendei haki hata kidogo maana sijawahi hata kuwa na wazo naye,” alisema Husna Maulid.

1 comment:

Anonymous said...

Pole dada,hujui watu rahisi kuwaza ngono kuliko kufikiri vingine? Haukuwa na umuhimu kujihami kwao kwani mwisho wa siku ukweli wako uko kwa Mola pekee. Songa mbele watz!!!!majungu hayana mshiko. Dada endelea tu na mahusiano na yeyote utakayeamua,iwe mapenzi,business zote hazituhusu!!! Best of luck!!!