Jukwaa la Katiba Tanzania limeshindwa kwenda mahakamani kama lilivyokuwa limepanga kufungua kesi dhidi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kwa kile ilichosema jopo la mawakili wake linaendelea na kazi ya uandaajia wa hoja za kuifikisha mbele ya sheria tume hiyo.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba, akizungumza na NIPASHE jana, alisema siku ya jana walikutana na mawakili hao na kujiridhisha na mwenendo wa kazi wanayoifanya na kwamba sasa Mei 22 watakwenda mahakamani kutimiza azma yao. Alisema suala la kwenda mahakamani ni la Watanzania wote kwa kuwa Katiba inayopiganiwa ni kwa ajili yao, hivyo siku hiyo kutakuwa na idadi kubwa ya watu kwenye mahakama hiyo watakaofika kushuhudia.
Kibamba alisema uamuzi wa kwenda mahakamani unatokana na jukwaa hilo kupuuzwa na mihimili ya Bunge na Serikali na wasaidizi wa Rais kuwakataza kuonana na Rais, kwa ajili ya kuwasilisha maoni yao na kuona njia pekee ya kutafuta haki ni kwenda mahakamani.“Tunaenda mahakamani kuomba isimamishe mchakato wa Katiba mpya hadi watakapoona umuhimu wa kuheshimu na kufuata ratiba waliojiwekea, kuheshimu misingi ya uandikaji na iamuru kusimama kwa mchakato huo,” alisema.
Alianisha kasoro ni mchakato huo kupelekwa kwa kasi inayoathiri misingi mikuu ya ujenzi wa Katiba mpya kwenye uelewa na hamasa, ushiriki, umiliki wa wananchi na hivyo mchakato huo unaweza kuzaa Katiba isiyo na sauti na maoni ya Watanzania wote.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment