ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 2, 2013

Kesi dhidi ya Lwakatare yazidi kupigwa kalenda

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  imeahirisha kesi ya ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick.

Kesi hiyo iliahirishwa juzi na Hakimu Aloyce Katemana,  baada ya Wakili wa Serikali, Peter Maugo, kuiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika ila jalada la kesi hiyo lipo polisi.


Hakimu Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 13, mwaka huu kwa ajili ya kwenda kutajwa tena hadi  jalada litakaporudishwa mahakamani.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mulungu, alisema upelelezi umekamilika na  jalada linaandaliwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi.
.
Lwakatare na mwenzake, Ludovick, wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama, kufanya mipango ya kumteka na kutaka kumdhuru kwa sumu, Dennis Msacky.
CHANZO: NIPASHE

No comments: