Thursday, May 23, 2013

KIJANA ALIYEUAWA KWA KUPIGWA RISASI KATIKA VURUGU ZA MTWARA, PAMOJA NA MADHARA NA HALI ILIVYO SASA HII HAPA

RIP Kaka Karim(Picha Mpasta, JAMII FORUMS)
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aapa kupambana na hao wanaofanya vurugu.
Nyumba ya Mtangazaji wa TBC yachomwa moto.
Ofisi ya Mbunge wa Mtwara/Mikindani imechomwa moto..
Nyumba ya Polisi imechomwa moto
Maaskari 10(awali walisema 4) wa kikosi cha JWTZ Nachingwea wamefariki dunia kwa ajali baada ya gari lao kupinduka maeneo ya Kilima hewa walikuwa wanakuja kuongeza nguvu Mtwara. Majeruhi wengi wao wamekatika viungo.
Nyumba za Hawa Ghasia zilizopo Indian quarterz(Sio India Quarters ni maeneo ya Kiyanga) zimechomwa moto
Gari la Zimamoto lapata ajali katika jitihada za kwenda kuzima moto
Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA 
Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa) 
Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela
Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake
Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.SOURCE http://mtwarakumekucha.blogspot.com/

2 comments:

Anonymous said...

Hapa ndipo CCM ilipotufikisha... Siku zote serikali haitaki kusikiliza wananchi: ( Mnadhani nguvu ya dola ndiyo suluhisho.. Vijana wamechoshwa na ubabe wenu, umasikini wa kupindukia Mtwara.. vijana hawana kazi kwa nini mnalazimisha kusafirisha gesi? Mtawafunga na kuwaua wangapi? Hata mkiwaua mtawamaliza? Mchawi yumo ndani ya CCM msitumalizie vijana ni uhai wa Taifa ...Siku zote mnaamini ktk kulazimisha hoja zenu kwa nguvu ya dola.. kwa nini msikubali gesi izalishwe Mtwara? ....

Anonymous said...

Ni mawazo na ushauri wa ajabu kufikiri ni CCM ndiyo iliyotufikisha hapa. Je wale wanaohusisha suala la maliasili gesi na siasa za kujuchukulia nchi kiutawala unawasemaje. Endapo CCM itaondoka madarakani utatatua suala hili vipi? Kuna dalili kuwa hata Zanzibar moto wa vurugu miaka ya nyuma ulichangiwa na wachangiaji wakubwa wa vurugu hizi za leo. Shinyanga kunaendelea kuchimbwa almasi,dhahabu na tangu awali hakujatokea vurugu kuwa watu wa Shinyanga wakadai maendeleo kwa ardhi yao kuwa na Raslimali hizo, narudia watu wa Shinyanga si wajinga bali ni watanzania halisi tena kabla hata Tanganyika haijawa huru, Wote tulio na tunaosikia siasa za Nigeria tufungue masikio zaidi, kuna watu wanaburuzwa kutenda wanayoyatenda na watu ambao Serikali inawalinda kwa kuwa ni wanasiasa na halafu wao hao wanaichagiza serikali kwa ilani zake za uchaguzi.Ni sumu mbaya tunakokwenda angalia dalili, kuvunja daraja lililo kwenye ilani ya uchaguzi ulopita ni unyama kwa wananchi hao hao unaowatia munkari kuichukia serikali yao.Kama raia hawana vita na polisi na kama wanaheshimu mihimili ya sharia kwa nini wachome vituo vya polisi. Democracy ikitumiwa vibaya na wale wanaoijua madhara yake ni makubwa tuwe makini. Kuna uwezekano kuwa kwa kuwa Tanzania haikuwa na mtu makini wa kuishitaki kwa mabwana wa nje sasa Watanzania wachache wenye wivu wa kilafi wanaona mwanya ili kuichafua Tanzania. CCM haina pesa za kujenga bomba la gesi ni wawekezaji ambao huogopa vurugu. Tukishawatisha hatutaweza kuwaita tena,Mtwara amkeni,Wanao chagiza vurugu kuweni wazalendo kuongoza ni zaidi ya uroho wa madaraka na chochote kinachotokana na kuhodhi ofisi kubwa yoyote katika taifa letu. Tanzania inaelekea kubaya tutumie busara na elimu kidogo kuwa makini kukemea maovu ambayo tunayaona kuendelea kutokea. Hii yote ni sumu ambayo Baba wa Taifa aliiona kwa mtazamo wake wa ubaguzi. Ukishaanza kumega nchi kwa ajili ya bomba la gesi, itabidi uimege zaidi kwa Korosho,Kahawa, Samaki,Ng'ombe na madini mengine niliyo yataja awali. Ikibidi Mtwara waachiwe gesi yao mpaka watakapo soma somo na Tanzania iangalie yale ya Nigeria,Sudan yasitokee maana kuna watu wako tayari kutuvunja kwa gharama yoyote na kutumia wachache ambao wako mguu ndani mguu nje Tanzania.Ninatabiri kwa mwendo huu Tanzania inamegeka. Mungu ibariki Tanzania Maliasili Laana isitukumbe.