ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 30, 2013

KINANA AWAONDOA HOFU WAKAZI WA ZIWA NYASA

Mbunge wa Ludewa ,Ndugu Deo Filikunjombe akizungumza na wakazi wa shina la Nileni na kuwaambia masuala ya ujenzi wa barabara na kituo cha afya. 
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana,akiwa na mbunge wa Ludewa,ndugu Deo Filikunjombe,wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Lupingu,Wilaya ya Ludewa ambapo Katibu Mkuu aliahidi kusaidia mabati500 na mifuko 700 ya cement kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya. 
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana, Mbunge wa Ludewa,Deo Filikunjombe,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe,Deo Sanga,na mjumbe mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe,Pindi Chana wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakazi wa kijiji cha Nindi wilaya ya Ludewa. 
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,wakiongozana na wabunge Deo Filikunjombe wa Ludewa na Kange Lugora wa Mwibara kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa katika kijiji cha Lupingu ambapo Katibu Mkuu aliwaondoa hofu wakazi wa kijiji hicho kwa kuwaambia hakuna vita itakayotokea. 
Picha na Adam H. Mzee

No comments: