ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 30, 2013

KINANA :CCM KUTEKELEZA AHADI ZOTE KWA WAKATI


Kikundi cha Sanaa cha SUMASESU cha kijiji cha Ukwama kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara,tarehe 30 Mei 2013.

Mkuu wa Wilaya ya Makete Ndugu Josephine Matiro akisalimia wananchi wa kijiji cha Tandala wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi , Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Ukwama na kuwataka wananchi wa kijiji hicho wasidanganyike na kukubali kugawanywa na waroho wa madaraka.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Ukwama na kuwaambia wananchi kuwa wae makini na chuki inayopandikizwa hivi sasa na kuwataka washikamane katika kutunza umoja na amani waliyonayo.
Wanakwaya wa Kijiji cha Iniho kata ya Iniho tarafa ya Magome wakitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa wakati mbele ya wakazi wa kijiji cha Iniho.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Iniho ambapo alisisitiza chama cha Mapinduzi ndio chama pekee kwa sasa nchini chenye uwezo wa kudumisha na kujenga umoja wa Watanzania na kuhakikisha kila mwananchi anaishi kwa amani.
Mbunge wa Makete, Ndugu Binilith Mahenge akihutubia wananchi wa kijiji cha Iniho ,ambao aliweza kueleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi unavyoenda vizuri katika wilaya yao ikiwa pamoja na kujengwa kituo cha afya ,pia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na kufikisha umeme kwa wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Iniho ambapo alisisitiza CCM inasimamia vizuri utekelezaji wa ilani yake na yale yote ambayo CCM iliahidi yatakamilika kama ilivyopangwa, pia alisema viongozi wa CCM wasisite kutoa taarifa kila mara kwa wananchi wao .
Wananchi wa Kijiji cha Iniho,tarafa ya Magome wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

Picha na Adam H. Mzee

No comments: