Monday, May 27, 2013

LADY JAYDEE ATOA ALBUM YAKE BURE

Katika kile kinachoonekana kama kuongeza msisimko katika tamasha lake la kutimiza miaka 13 ya muziki wake na uzinduzi wa albamu yake ya sita tangu kuanza muziki, mwanamuziki Lady Jaydee ametangaza rasmi kwamba kila atakayehudhuria onyesho lake na kulipa kiingilio, atatoka na nakala ya albam yake hiyo albamu ya bure.

Akiiongelea albamu yake hiyo aliyoipa jina la 'Nothing But The Truth', amesema si albam ambayo kijana aliye katika harakati anapaswa kuikosa, maana humo ndani ameelezea kwa kiasi kikubwa changamoto za kimaisha na jinsi ya kukabiliana nazo kama kijana.

Jaydee maarufu pia kwa jina la 'Anaconda' usiku huo atasindikizwa na Joh Makini, Grace Matata, Profesa jay, Hamza Kalala na bendi yake ya Machozi Band.

No comments: