ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 27, 2013

Lema amvaa Lowassa kwa helikopta Monduli

Monduli. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema jana aliongoza kampeni za Chadema za udiwani katika Kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli kwa staili ya aina yake, akitumia helikopta huku ikidondosha vipeperushi vya mgombea wa chama hicho, Japhet Sironga.
Akizungumza katika kampeni hizo, Lema alisema: “Chama chetu kina uhakika wa ushindi kwani Sironga ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Ilboru, ana uwezo mkubwa kwa kuwa ni msomi.
Lowassa ndiye aliyepewa mikoba na CCM ya kumnadi mgombea wa chama hicho na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wabunge wa chama hicho Mei 19, mwaka huu Mjini Dodoma alisema kiongozi huyo anatosha kukipa ushindi katika kata hiyo.
Lema alisema: “Makuyuni, hamna maji, hamna huduma za afya, hakuna barabara za vijiji, wafugaji ardhi yenu inaporwa sasa ukombozi wenu umefika kama mkimchagua msomi Sironga.”
Alimkabidhi mgombea huyo taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kumtaka kazi yake ya kwanza iwe kuibua ufisadi na kumfikishia bungeni ili kuiokoa Halmashauri ya Monduli.
Akizungumza katika kampeni hizo, Sironga alisema ameamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho, ili kuokoa jamii ya Makuyuni na Monduli kutokana na shida zinazowakabili.
ADC Kigamboni
Chama cha ADC kimezindua kampeni ya nyumba kwa nyumba ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mianzini, Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Kigamboni, Mwenyekiti wa ADC Wilaya ya Temeke, Salum Sudi alisema kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi  ikiwamo kero ya maji, barabara, elimu ya msingi na soko, hivyo wakipewa ridhaa hiyo kero hizo zitakwisha...
Nyongeza na Pamela Chilongola.
Mwananchi

No comments: